.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, March 29, 2013

KIKWANGUA ANGA CHA GHOROFA 16 CHAPOROMOKA DAR. CHAUA, CHAJERUHI, CHAHARIBU

Rais Jakaya Kikwete pamoja na Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Goodluck Ole Madeye wakiwasili katika eneo la tukio jijini Dra ambako jengo la ghorofa 16 lililokuwa likiendelea kujengwa limeporomoka na kuua watu, kujeruhi na kuharibu mali.

Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia ambaye ni mtaalam wa mambo ya majanga kama haya kwenye eneo la tukio



Rais akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam. Rais ameagiza wahusika wawajibishwe


Mtaalam wa Majanga Mhe. James Mbatia akielekeza cha kufanya


Baadhi ya mali zilizoharibika


Jengo lililoko pembeni mwa lililoporomoka ambalo linaendelea kujengwa kama inavyoonekana na inasemekana mkandarasi wake ni mmoja na aliyejenga jengo lililoporomoka


BURIANI MHE SALIM HEMED KHAMIS


Mharehemu Salim Hemed Khamis Mbunge wa Chambani Pemba aliyefariki dunia tarehe 28/3/2013 baada ya kuugua kwa muda mfupi


Viongozi wote wa kitaifa, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis katika ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam mara kabla ya kuanza safari ya kuelekea Chambani Pemba kwa mazishi.


Wednesday, March 27, 2013

SPIKA AITAKA TAKUKURU KUWA NA MENO

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimsiliza kwa makini Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bi Mary Mosha (kulia) kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Tanzania (TAKUKURU) alipokuwa akitoa maelezo mafupi pamoja na kuutambulisha ujumbe wa Maafisa Waandamizi wa chombo cha kupambana na rushwa kutoka nchini Misri. Ujumbe huo ulioongozwa na Balozi wa Misri hapa nchini, Mhe. Hossam Moharam, upo Tanzania kwa nia ya kubadilishana uzoefu na TAKUKURU


  Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini Misri Jenerali Moustafa Raafat Abdel Salam (wa pili kushoto – wa kwanza ni Balozi Moharam) akimwelezea Spika Makinda hatua zinazochukuliwa na taasisi yake katika kupambana na rushwa nchini Misri.

   Ujumbe huo ukiwa katika meza ya majadiliano


   Sehemu ya ujumbe huo.



Tuesday, March 26, 2013

KIKWETE AFUNGA MAFUNZO YA JKT KWA WABUNGE

Wabunge wkila kiapo cha uzalendo mara baada ya mafunzo ya muda mfupi ya JKT

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mufunzo hayo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Bulaya katika Kambi ya Ruvu jana

Monday, March 25, 2013

XI JINPING AUTANGAZIA ULIMWENGU SERA ZAKE KWA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping akimkadidhi Rais wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete funguo za jengo la mikutano ya Kimataifa la Mwalim Nyerere lililojengwa kwa msaada wa China leo tarehe 25 Machi 2013 Jijini Dar se Salaam


Rais Kikwete akimkaribisha mgeni wake


Rias Xi Jinping akiutangazia ulimwengu sera zake kwa Afrika ambapo amesema uchumi ni kipaumbele cha kwanza


Kutoka kushoto: Mama Salma Kikwete, Rais Xi Jinping, Rais Kikwete na Mama Peng Liyuan (mke wa Rais wa China)

Rais Xi Jinping alikutana na Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Ali Mohamed Shen katika Hotel ya Serena na kuwa na mazungumzo mafupi


Baadaye viongozi hao walielekea eneo la Majohe -Gongo la Mboto, nje kidogo ya jiji penye makaburi ya wataalam wa kichina waliofariki dunia wakati wa kuijenga reli ya TAZARA na kuweka mashada ya maua katika makaburi hayo.


Mama Peng Liyuan na Mama Salma Kikwete wakiweka mashada ya maua. Baada ya shughuli hiyo Rais Xi Jinping na ujumbe wake walihitimisha ziara hiyo ya siku mbili na kuondoka kwenda Afrika ya Kusini .

Friday, March 8, 2013

RWANDA YAIOMBA TANZANIA KUIMARISHA MAHUSIANO

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ben Rugangazi, wakati Balozi huyo alipomtembelea Spika ofisini kwake Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo yao, Balozi Rugangazi alimuomba Spika kupitia Bunge nchi mbili hizi zizidi kuimarisha mahusiano mzuri yaliyopo.
Spika Makinda alimhakikishia Balozi Rugangazi kulisimamia jambo hilo huku akimweleza kwa muhtasari nia ya mabadiliko ya Bunge ya kuanza mkutano wake wa Bajeti mwezi Aprili badala ya mwezi Juni kama ilivyozoeleka. Mkuu huyo wa mhimili wa Bunge amesema hatua hii itaisaidia serikali kuanza kutumia fedha za mapato na matumizi mara tu mwaka wa fedha wa serikali (Julai Mosi) unapoanza. "Siku ya kusomwa bajeti kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itabakia kuwa ni ile ile ila sisi tutaanza kujadili wizara zote za kisekta isipokuwa wizara ya Fedha hadi mwezi Juni," alisema Spika na kuongeza.
Balozi Rugangazi aliifurahia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa Rwanda inayo mengi ya kujifunza kutoka Tanzania. Aidha Balozi huyo alitoa mwaliko na taarifa ya maadhisho ya siku ya 'Utu wa Binadamu' ambayo taifa la Rwanda huadhimisha kila tarehe 7 Aprili kwa ajili kuwakumbuka wale wote waliouawa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu takriban milioni moja waliuawa kikatili kufuatia mchafuko baina ya kabila la Wahutu na Watutsi.

Thursday, March 7, 2013

Mvua za Dar


Utii bila shuruti


Kibanda akimbizwa Afrika Kusini

Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania Bw. Absolon Kibanda akiingizwa kwenye
ndege maalum tayari kukimbizwa Afrika Kusini baada ya kuvamiwa na
 kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana


Wadau wa habari waliofika Muhimbili alikokuwa amelazwa Mhariri Mkuu wa
 Gazeti la Mtanzania

WAZIRI MKUU WA DENMARK ATUA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni
wake Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning - Shmidt (kushoto)


Rais na mgeni wake wakiwasili Ikuku