.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Thursday, April 10, 2014

JK Kiongozi Bora Afrika 2013

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe  (katikati) akipokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kiwete Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 kutoka kwa Balozi wa Nigeria nchini Marekeni Profesa Adebowele Adufye. Tuzo hiyo imetolewa tarehe 9 Aprili 2014 katika Hotel ya St. Regis jijini Washington DC. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye alikuwa nchini Marekeni kikazi na hivyo akaalikwa kwenye hafla hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (katikati) akimkabidhi Naibu Spika Mhe. Job Ndugai Tuzo hiyo maalum. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na kulia kabisa ni Balozi Adebowele Adufye

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akinyanyua Tuzo hiyo juu

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiinyanyua juu Tuzo hiyo

Waziri Membe akiifurahia Tuzo

Kwaya maalum iliyotumbuiza wakati wa utoaji wa Tuzo hiyo.

Tuesday, April 8, 2014

Dar in the making....

Ubungo

Kimara


Manzese

Magomeni

Rwanda yaadhimisha miaka 20 mauaji ya Kimbari tarehe 7 Aprili

Viongozi mbalimbali wakiwasili jijini Kigali, Rwanda

Katibu Mkuu wa Chama cha RPF Bwana Francois Ngarambe akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Bwana Abdulrahman Kinana alipowasili Kigali kuiwakilisha Tanzania

Kutoka kushoto ni Bwana Kinana, Bwana Ngarambe na Mjumbe wa NEC Balozi Ali Karume 

Katibu Mkuu Kinana akitoa neno la shukrani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Bwana William Hague akibadilisha mawazo na Katibu Mkuu Kinana

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Bwana. Thabo Mbeki akisalimiana na Bwana Kinana

Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Botswana Bwana Ketumile Masire, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Bwana Benjamin William Mkapa, Mama Anna Mkapa na Katibu Mkuu wa CCM Bwana A. Kinana

Rais wa Kenya Bwana Uhuru Kenyatta na Katibu Mkuu wa CCM Bwana Kinana

Kutoka kushoto ni Mstaafu wa Burundi Bwana Pierre Buyoya, Mama Buyoya na Bwana Kinana

Wednesday, April 2, 2014

Bunge la Afrika Mashariki lachafuka, laahirishwa


ARUSHA,Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limeanza kuonekana kufanana na Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Bunge hilo jana limevunjika bila kujulikana litakutana tena lini baada ya kuibuka mabishano ya kisheria kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Spika, Margret Zziwa.
Hoja ya kumng’oa Spika Zziwa ilianza kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa na hatimaye kuwasilishwa jana na Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya kwa niaba ya wenzake Shy-Rose Bhanji wa Tanzania, Nyiranilimo Odette wa Rwanda na Hafsa Mossi kutoka Burundi.
Awali Bunge hilo linalopaswa kuanza vikao vyake saa 8:00 mchana lilichelewa kuanza hadi Saa 9:44 alasiri baada ya wabunge kugoma kuingia ukumbini walipobaini kuwa hoja ya kumng’oa Spika haikuwa miongoni mwa shughuli za Bunge kwenye kikao cha jana.
Baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya ofisi ya spika, Mwanasheria wa EAC, Wakili Wilbert Kaahwa na Katibu wa Bunge, Kenneth Madete, Spika Zziwa alikubali hoja ya kumng’oa iongezwe kwenye orodha ya shughuli za Bunge ndipo Mbunge Mathuki alipopewa fursa ya kuwasilisha hoja.
Hata hivyo dakika moja tangu Mathuki alipoanza kusoma maelezo ya hoja hiyo, Mbunge Fred Mukassa Mbidde aliinuka na kuomba mwongozo wa Spika na alipopewa nafasi, alipinga hoja hiyo kuwasilishwa na kujadiliwa kwa madai kuwa kuna kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) inayohusiana na hoja hiyo.
Akifafanua Mbidde alisema kesi hiyo inaomba mwongozo na ufafanuzi wa kisheria kuhusu kanuni ya 9 ya Bunge la EAC inayoelekeza utaratibu wa kumwondoa madarakani Spika wa Eala iwapo kutatokea haja ya kufanya hivyo.
Wakati Mbunge Mbidde akiwa bado amesimama huku akiendelea kutoa hoja yake, Mbunge Joseph Ombasa kutoka Kenya aliinuka na kumpinga mbunge mwenzake akisema anataka kulipotosha Bunge kwani kifungu 38 (3) kinaruhusu Bunge hilo kujadili hoja yoyote yenye masilahi ya umma wa EAC ikiwamo hilo la kumng’oa Spika.
Baada ya hoja ya Ombassa, Mwanasheria wa EAC, Kaahwa alisimama kutoa ufafanuzi wa kisheria licha ya kukiri kuwapo kesi mahakamani alisema tayari mahakama hiyo imetoa uamuzi mdogo kuwa shauri hilo haliwezi kuzuia shughuli na mjadala wowote wenye nia ya kumwondoa Spika madarakani
Hoja hiyo ya Mwanasheria ilimwibua tena Mbunge Mbidde aliyehoji kwanini maelezo na ufafanuzi wa mwanasheria huyo yanatoa mwelekeo wa ulipo msimamo wake kuhusu hoja iliyokuwa mbele ya Bunge.
Katika hali iliyoashiria uwapo wa kimkakati kati ya kiti cha Spika na Mbunge Mbidde, Spika Zziwa naye aliunga mkono hoja ya mwanasheria kuonekana anaelemea upande unaotaka ang’olewe.
Kauli hiyo ilimwamsha kitini Mwanasheria Kaahwa aliyemhakikishia Spika kuwa hoja yake inalenga kusaidia uendeshaji bora wa Bunge na siyo kuegemea upande unaotaka kumng’oa.MWANANCHI


Chini ni saini za wabunge za kumwengua Spika