.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, March 30, 2015

Wizara ya Ujenzi ilikotoka, iliko na inakokwendaJK awasili USA kwa mwaliliko wa Umoja wa Mataifa, afungua jengo la Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa


Ni jengo la ghorofa sita


Ni mabalozi waliowahii kuuongoza uwakilishi huu


Akisalimiana na viongozi

Akikata utepe wa Jengo


Makandarasi waliojenga hicho kikkwangua angaMwakilishi wa kudumu Balozi Tuvano Manongi akishuhududia Mhe. Rais akisaini kitabu cha wageni
Akisalimiana na watanzania waishio USA

Picha za Pamoja

Utamaduni mpya wa mahubiri....... Gwajima, Kakobe....... matusi, vijembe, Mipasho...... Kardinali Pengo ametufundisha kusamehe.....


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
29/03/2015
WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao hivyo waliwakatalia kuingia.
Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa kundi hilo.
Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa na Begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya PUMAChaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi, Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24, Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62, Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30, Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva, Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60, Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39, Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Saturday, March 28, 2015

JK akamilisha uteuzi wa wabungeHatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekalisha uteuzi wa wabunge kwa mujibu wa ibara ya 66 kifungu (1) aya ya (e) ya  Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayompa mamlaka ya kuteua watu wasiozidi kumi (10) kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Katika uteuzi huu Rais amemteua Dkt. Grace Puja na Ndugu Innocent Sebba kuwa wabunge na tayari Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) amewaapisha ili waweze kuanza kazi rasmi.

Wabunge walioteuliwa na Rais kwenye Bunge la Kumi kwa mujibu wa Katiba ni wafuatao:
1.     Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhango
2.     Mhe. Dkt. Asha-Rose M. Migiro
3.     Mhe. Saada Mkuya Salum
4.     Mhe. James Francis Mbatia
5.     Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
6.     Mhe. Janet Zebedayo Mbene
7.     Mhe. Zakia Hamdani Meghji
8.     Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
9.     Mhe Dkt. Grace Khwaya Puja na
10. Mhe. Innocent Rwabushaija Sebba

Kwa uteuzi huu idadi ya wabunge imetimia 357 kikatiba
Mteule Innocent Sebba akila kiapo cha utii

Spika Makinda akikabidhi vitendea kazi kwa Mbunge mteule Innocent Sebba. Anayeshuhudia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashillilah

Wednesday, March 25, 2015

Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama wenye majeshi na polisi kwenye opereshini za kulinda amani zilizo chini ya Umoja wa Mataifa wamekutana kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York na kufanya mkutano wa kihistoria. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwasili kuufungua mkutano huoCDF Mwamunyange, ujumbe wake na maafisa Ubalozi

Uingereza, Malawi zukutana Dodoma

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda alipokutana na Baroness Lindsay Northover, Waziri wa masuala ya Bunge la Uingereza

Spika Anne Makinda akiendesha kikao cha Tume ya Utumishi wa Bunge ya Malawi ilipotembelea Dodoma hivi karibuni (24/3/15)