.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, January 28, 2014

Spika Ziarani Wellington, Geneva


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) anatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015. Kamati hiyo inayoundwa na  Maspika 37 walioteuliwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge Duniani Mjini Geneva. Mkutano wa pili wa Kamati hiyo ya Maandalizi utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Aidha, kabla ya kwenda Geneva, Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika Wellington, New Zealand kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2014.

Kwa ujumla, ushiriki wa nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri ya kuitangaza na kuipa heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa jukwaa madhubuti linalotumika kuiweka nchi katika ramani ya dunia na kuonyesha vivutio hususan katika nyanja za uwekezaji, utalii na maliasili pamoja na fursa mbalimbali zilizomo.


Imetolewa na:

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
28 Januari 2014

Monday, January 27, 2014

Habari mchanganyko

Mikutano ya Chadema


Mwana mama akimsadia dereve wa Bajaji kubadilisha tairi

Ndege yakosa breki na kwenda porini huko Zanzibar

Mikutano ya CCM


Rais wa Madagascar Henry Rajoarinamampianina aapishwa 


Waziri Membe akimuwakilisha Rais Kikwete Madagascar kwenye kuapishwa kwa Rais

Viongozi wa juu wakiteta jambo