Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimsiliza kwa makini Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bi Mary Mosha (kulia) kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) alipokuwa akitoa maelezo mafupi pamoja na kuutambulisha ujumbe wa Maafisa Waandamizi wa chombo cha kupambana na rushwa kutoka nchini Misri. Ujumbe huo ulioongozwa na Balozi wa Misri hapa nchini, Mhe. Hossam Moharam, upo Tanzania kwa nia ya kubadilishana uzoefu na TAKUKURU
|