.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Sunday, February 26, 2012

Spika Makinda aongoza maelfu kumuaga marahemu Mnyanga


Viongozi wa dini wakijiandaa kwa ibada ya kumuaga aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali Watu na Mshauri Mkuu wa mambo ya Utawala  wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  marehemu Leo Theodore Mnyanga aliyefariki dunia tarehe 22 Feb. 2012 na kuzikwa katika makaburi ya Mlima Kola nje kidogo ya mji wa Morogoro leo tarehe 26 Feb.  2012.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaongoza waombolezaji  kwa kutoa salamu za rambirambi katika mazishi hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndugu Joel Bendera (kushoto), Spika Makinda na Mhe. Bura (kulia) wakimfariji mke wa marehemu (katikati).


Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ngugu Jossey Mwakasyuka akimwakilisha Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah katika kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa ofisi ya Bunge.


Familia ya marehemu ikitoa heshima za mwisho kwa baba yao mpendwa.

Wafanyakazi wa ofisi ya Bunge wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mnyanya kuelekea makaburini.

Spika Makinda akiweka udongo kaburini.

Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro Ndg. Joel Bendera akiweka shada la maua juu ya kaburi.

Watoto wa marehemu (Fred-aliyshika picha na kaka yake) wakitoa neon la shukrani kwa waombolezaji.

Friday, February 10, 2012

Balozi Mulamula atembelea Bunge Dodoma

  Katibu Mtendaji wa jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu aliyemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula (kulia) akisalimiana na kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Bungeni Dodoma leo.

Balozi Mulamula (kulia atika viwanja vya Bunge Dodoma) akisalimiana na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) leo k leo.


Spika Makinda akifurahia jambo na Mbunge wa Simanjoro Mhe. Ole Sendeka (kati) na mdau wa michezo Wakili  Imani Madega.



Balozi Mulamula (kulia) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb) mjini Dodoma leo. Balozi Mulamula alifika Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo.

Balozi Mulamula akiwa na afisa wa Bunge Bw. Prosper Minja mara kabla ya kuanza kwa kiako cha Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.

Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe akisalimiana na afisa wa Bunge