.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, August 30, 2016

Matukio mbalimbali

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili nchini Swaziland ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kuhudhuria Mkutano wa 36 wa SADC Agosti 28, 2016

Mapokezi ya Makamu wa Rais

Vikundi vya Ngoma

Makamu wa Rais akifanya mazungumzo na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Swaziland

Jengo unamofanyoka Mkutao wa 36 wa SADC

Raia wakishangaa ajali iliyosababishwa na Dadadala huko Temeke leo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akijadili jambo na ujmbe wa japani hapa nchini

Tukio la kihistoria: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (JPJM) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mgombea Urais kwa tiketi ya muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutipa CHADEMA Mhe. Edward Ngayai Lowassa. Hii ni mara yao ya kwanza wanakutana na kusalimiana tangu Mhe. Lowassa alipotoka CCM na kuhamia CHADEMA mapema mwezi Juni mwaka 2015. Vingozi hawa walikutanishwa na tukio la sherehe ya miaka 50 ya jubilee ya ndoa ya Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa tarehe 27/8/2016 Jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilitoke wakati nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya kiusalama kufuti mvutano mkubwa kati ya CHADEMA, Polisi na katozo la Rais la mikutano ya vya vya siasa. CHADEMA tayari imetangaza maandamano nchi nzima kwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) tarehe 1/9/2016 na Polisi tayari imeyapiga marufuku maandamano hayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bwana George Masaju akuzungumza na vyombo vya habari kuhusu uharamu wa UKUTA

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania Bw. Augustino Lyatonga Mrema akionge na vyombo vya habari kuhusu vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Waziri wa Habari Utamaduniu na Michezo Mhe. Nape Moses Nauye akifafanua jamabo baada ya kutangaza kuvifunga vituo vya radio vya Radio 5 na Magic FM kwa makosa ya uchochezi na kashfa kwa Mkuu wa nchi mapema tarehe 29/8/2016

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Kulia) akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwenye Mkutano wa Japan - Africa Business Conference Jijini Nairobi Agosti 27, 2016

Picha ya pamoja kwenye Japan - Africa Business Conference Nairobi