.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, May 31, 2011

Kuelekea Katiba Mpya: Spika Makinda akutana na BAKWATA, Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania

     Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba akimkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Ofisini kwakeDar es Salaam leo. Spika Makinda alifanya ziara hiyo kwa lengo la kupanua mjadala wa maudhui ya kuundwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya. Kulia kwa Mufti ni Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaji Suleima Lolilya na kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki. Aidha Spika Makinda pia alikutana na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania kwa mwaliko wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kupokea maoni na ushauri kuhusu uundwaji wa chombo hicho cha kukusanya maoni.

     Mufti Mkuu akiendesha Dua maalum kabla ya mjadala kuanza.


      Viongozi wa BAKWATA wkifuatilia mjadala.

      Mufti akitoa maoni yake.

  Spika Makinda akiushikuru uongozi mzima wa BAKWATA na kuwaahidi kuwa maoni na ushauri wao vitazingatiwa

     Spika Makinda (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania katika Hotel ya Courtyard, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekit wa Baraza na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza.

     Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji akimshukuru Mhe. Spika kwa uamuzi wake wa busara wa kukutana na wadau mbalimbali ili kupata muafaka wa kitaifa wa upatikanaji wa katiba mpya


   Wajumbe wa Baraza wakifuatilia mjadala


   Baraza la vyama vya Siasa Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Anne Makinda (katikati)
Picha na Prosper Minja-Bunge

Monday, May 23, 2011

Matukio Bungeni


 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Anne Makinda akifafanua kwa wanahabari mwenendo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12 mara baada ya kufunga mkutano wa vyombo vya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali barani Afrika Ubungo Plaza Dar es Salaam, jana.


Mwenyekiti wa Kamati yaBunge ya Hesabu za Serikali Mhe. John Momose Cheyo Mb, akimkabidhi Mhe Spika zawadi iliyotolewa na wajumbe wa mkutano huo.



 Spika Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation, TPSF) Bi Esther Mkwizu akitoa maoni ya makundi mbali mbali ya wadau wa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya leo katika ofisi ya Spika wa Bunge. Kushoto kwake ni Spika Makinda akimsikiliza kwa makini.
Wajumbe kutoka TCCIA na TPSF wakifuatilia mjadala
Katibu Mkuu wa Baraza la wafanyakazi Tanzania Bw, Mgaya amabaye ameongozana na viongozi waandamizi wa vyama vya wafanyakazi vya CWT, TUGHE, RAAWU, TALGWU, TUICO, TUCTA na ATE akitoa maoni kuhusu kuundwa kwa tume ya Katiba mpya leo.

 Ujumbe kutoka Muungano wa Ulaya ukiongozwa na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Bw. Nick Westcott (kati) na Mwakilishi wa Muungano huo hapa Tanzania Balozi Tim Clake (kulia) ulipomtembelea Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda (kushoto) ofisini kwake leo. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamezungumzia uboreshwaji wa bajeti na mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Na Prosper Minja-Bunge



CCBRT for expansion and CPA Boss visits Tanzania


CCBRT Deputy Chief Executive Officer Ms Haika B. Mawalla (left) gives presentation of the expansion of the CCBRT Hospital to the Speaker of the Parliament of Tanzania Hon. Anne Makinda (right). Watching at the centre is Mr. Erwin Telmans the CCBRT Chief Executive Officer. The two paid Speaker Makinda a visit in her office today and request her, as the Patron of the Hospital, to officiate a fund raising function to be held for the expansion purposes.



Dr William Shija, the Commonwealth Parliamentary Association Secretary General,together with his wife Mama Getrude Shija giving a message of condolence to Speaker Anne Makinda following the sudden death of her mother early this month. The couples visited Madam Speaker in her office today.



Dr. Shija (right) meets and discusses various CPA issues with the Clerk of the National Assembly of Tanzania Dr Thomas Kashililah in the latter’s office today. The CPA Boss is in the country for a work visit.


.Hon. Al-Shyma Kwegyir (centre) in a joint photo with CPA Boss Dr William Shija (right) and Dr. Kashililah (left). By Prosper Minja-Bunge

Thursday, May 19, 2011

NCCR-Mageuzi, CUF watoa maoni ya muswada wa Tume ya Katiba Mpya

1.    Viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi (kutoka kulia Bw James Mbati-Mwenyekiti, Samuel Ruhuza – Katibu Mkuu na Dkt Ndalichako Kessy-Mkurugenzi wa Mambo ya Nje) wakitoa maoni yao jinsi ya kuuboreshwa muswada wa  sheria ya kuunda tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya ofisini kwa Spika leo.



1.    Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda na Makamu Mwenyekiti wa Kamata ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki wamkisikiliza Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kwa makini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Pindi Chana akiongea wakati wa mjadala huo leo.
1.     
      Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakitoa maoni yao.
Na Prosper Minja-Bunge

Wednesday, May 18, 2011

Maoni ya TADEA






Rais wa Chama cha Siasa cha TADEA Bw. Lifa Chipata akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda rasimu ya maoni ya chama hicho yenye lengo la kuuboresha muswada wa sheria ya kuunda Tume itakayoratibu ukusanywaji wa maoni ya kutengeneza Katiba mpya Ofisini kwa Spika leo.