.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Thursday, May 31, 2012

Arusha yaileta Afrika Tanzania: Ni kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika

Mzee Mustapha Songambele akikata keki ya 87 ya siku ya kuzaliwa. Wa karimu naye ni mywife wake Bi Kondo

Viongozi wa Afrika - Arusha

AICC

AICC May 31, 2012

Sunday, May 27, 2012

Mhe. Vick Kamata atoa Baiskeli kwa walemavu mkoani Geita

 Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Vicky Kamata  akisalimiana na mtoto mwenye  ulemavu wa mguu tangu kuzaliwa mwenye umri wa miaka 15.

 
Mhe. Kamata akisalimiana na watu wenye ulemavu mkoani Geita, Bukoli

 
Baadhi ya baiskeli za walemavu ambazo ni msaada uliotolewa na Victoria Foundation inayaomilikiwa na Mhe. Vicky Kamata

 Watu wenye ulemavu wakifurahia baiskeli baada ya kupewa masaada huo mkubwa na Mhe. Vick Kamata

Picha na Yona Kirumbi - Bunge

Thursday, May 24, 2012

Elimu kwa vitendo shuleni iko wapi?


KATIKA moja ya hotuba za hayati  Baba wa Taifa Mwlimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuna baadhi ya mambo hapa nchini ukitaka kuyahoji lazima uwe na moyo mgumu kama wa mwendawazimu hivi.   Kwa sasa moja ya mambo hayo ni elimu: elimu ya awali; elimu ya msingi; elimu ya sekondari; elimu ya vyuo. Zamani ili shule ihesabike na hata kusajiliwa kama shule kuna mambo mengi yalihitajika likiwemo la uwanja wa michezo na shamba la shule. Siku hizi ni dhambi ya mauti kuzungumzia shamba la shule tena mzazi akikuskia achilia mbali mwalimu! Mwanafunzi ndiyo kabisa atatamani umwagiwe tindikali!

Siku hizi mtoto anafanyiwa kila kitu awapo shuleni. Kuna watu wa kufanya usafi ndani na nje ya vyumba vya madarasa, , kupika, basi la kumbeba na kurudisha nyumbani, akifika nyumbani kuna msaidizi/mfanyakazi wa nyumbani wa kumfulia hadi nguo za ndani, kumpikia, kumtandikia kitanda na kunyooshea nguo. Shuleni shamba darasa tena hakuna. Zamani katika orodha ya vifaa vya kwenda navyo shuleni jembe kilikuwa kifaa kimojawapo. Siku hizi dhubutu! Kiwanja cha michezo si sharti muhimu tena. Hali hii iko tangu shule ya awali hadi chuo kikuu! Ni dhahiri maandiko haya hayatabadilisha chochote kwa wakati huu lakini yataonekana ya maana Wachina watakapoanza kuchangamkia hata kazi za majumbani hapa Tanzania kwani wao wamefundishwa maana ya kazi kwa vitendo.

Serikali, wazazi, wadau wako wapi kudai na kuhimiza kazi za mikono katika shule zetu? Shule yoyote kabla ya kusajiliwa ioneshe japo shamba darasa mahali wanafunzi watajifunza kwa vitendo kupanda na kuvuna mchicha. Wanafunzi wafundishwe kufanya usafi kwa vitendo kwa mfano kufagia darasa, kuokota takataka, kukata kucha, kuosha sahani yake anapomaliza kula, kutoa buibui na nyinginezo. Wakiwa majumbani wajifulie ngou zao wenyewe, wafanye usafi, wajifunze kupika, wanyooshe nguo zao wenyewe, watengeneze bustani na kuzimwagilia inapobidi, wahimizwe maswala ya kiroho, kwa kifupi wafundishwe kuwajibika.

Jeshi la Kujenga Taifa ndilo lilikuwa limesalia ili kuziba ombwe hili. JKT halipo tena. Na hata ikitokea likawepo halitokuwa tena kama la opereshini miaka 30 (waliopita jeshini wanaelewa operesheni).   Ole wetu! Ole wa Taifa hili!.Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dkt. Joyce Ndalichako alinukuliwa akilalamika kwamba wanafunzi waliandika mashairi ya Bongo flavor kwenye mitihani! Kumbe waandike nini? Nyimbo za makuzi shuleni siku hizi hakuna tena. Nyimbo za kizalendo na ukakamavu ni historia mashuleni! Kibaya zaidi hata Wimbo wa Taifa  umebaki kuchezwa mkanda tu uliorekodiwa halafu  wanafunzi wanasikiliza! Mustakabali wa Taifa uko wapi! Tusipojenga msingi imara tusishangae nyumba kuporomoka kwani Walatini wanasema volenti non fit injuria! (lakijitakia halina madhara). Tumeyataka wenyewe!

Tuna wakaguzi waliosoma. Hivi hawa wanakagua nini? Mwandiko mzuri? Mwalimu kumaliza silabasi? Wadau nisaidieni. Mada ni pana. Mtoto huyu akimaliza shule (darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, shahada ya kwanza) anakuwa ni mzigo usiobebeka pande zote. Si kwa wazazi, si kwa serikali! Hawezi kufanya kitu chochote! Hajafundishwa kufanya hivyo! Hajalelelwa katika mazingira hayo! Hana pa kuanzia. Dhana ya kilimo kwanza kwake ni msamiati usio na mashiko. Likitokea la kutokea kwamba mzazi amefariki dunia huu unakuwa ni mwanzo wa mwisho wa mtoto huyu! Ataanza kujioanisha na mazingira  yatakayomfaa (to search for identity). Atayapata mazingira hayo  au kwa watumia dawa za kulevya kwa wavulana au kwa kupiga umalaya kwa wasichana. Hapa tusiulizane madhara yake nini.

Laiti mtoto huyu angelikuwa anajua kujitegemea japo kidogo tu angeyamudu maisha. Angekuwa mnyenyekevu. Kwa bahati mbaya kila mtoto anaota kwenda Ulaya tena kwa gharama yoyote ile. Mzazi atafanya kila linalowezekana na lisilowezekana, mtoto atahonga hata visivyohongeka ili mradi aende Ulaya! Kufanya nini? Sina jibu.

Sera ya elimu iangaliwe upya. Shule zote (binafsi na serikali) ziwekewe vigezo. Tusiogope kujifunza kutoka mahali pengine. Kwa mfano shule za seminari zinaongoza kwa kufanya vizuri. Lakini hapa ni mahali wanafunzi wanafanya kazi zote peke yao. Wana mashamba yao wanayolima na kuvuna wenyewe, wanafanya usafi wa mazingira na vyumba vya madarasa yao, kwa kifupi wanajitegemea wakiongozwa na nidhamu ya hali ya juu. Haijawahi kutokea mtoto aliyemaliza masomo katika shule hizi akawa tegemezi kiasi cha kutobebeka. (kwa ujasiri naruhusu changamoto/challenge kwa hili kutoka wa mtu yeyote). Huu ni ushahidi kwamba inawezekana.

Tujenge msingi imara ili kuwa na taifa imara.

0713 123 254
Wednesday, May 16, 2012

Mnadani Dodoma....kwa wageni na wenyeji... Bila kufika mnadani hujafika Dodoma

Wajasiriamali

kitoweo

manthariVinywaji


profile ya wateja/wadau

Mapumziko


Karibuni

Wednesday, May 9, 2012

Obama aialika Afrika G8Rais Barak Obama wa Marekani amewaalika viongozi wanne kutoka Afrika kuhudhuria Mkutano wa G8. Vingozi hao ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Rais Yayi Boni wa Benin, Rais Atta Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi. Mkutano huo utafanyika Camp David kuanzia Mei 19, 2012 

Wakuu wapya wa Wilaya

MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA 70 NA VITUO VYAO VYA KAZI

MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA 70 NA
VITUO VYAO VYA KAZI
NA.
JINA
KITUO  CHA KAZI
1.
Novatus Makunga
Hai
2.
Mboni M. Mgaza
Mkinga
3.
Hanifa M. Selungu
Sikonge
4.
Christine S. Mndeme
Hanang
5.
Shaibu I. Ndemanga
Mwanga
6.
Chrispin T. Meela
Rungwe
7.
Dr. Nasoro Ali Hamidi
Lindi
8.
Farida S. Mgomi
Masasi
9.
Jeremba D. Munasa
Arumeru
10.
Majid Hemed Mwanga
Lushoto
11
Mrisho Gambo
Korogwe
12.
Elias C. J. Tarimo
Kilosa
13.
Alfred E. Msovella
Kiteto
14.
Dkt. Leticia M. Warioba
Iringa
15.
Dkt. Michael Yunia Kadeghe
Mbozi
16.
Mrs. Karen Yunus
Sengerema
17.
Hassan E. Masala
Kilombero
18.
Bituni A. Msangi
Nzega
19.
Ephraem Mfingi Mmbaga
Liwale
20.
Antony J. Mtaka
Mvomero
21.
Herman Clement Kapufi
Same
22.
Magareth Esther Malenga
 Kyela
23.
Chande Bakari Nalicho
Tunduru
24.
Fatuma H. Toufiq
Manyoni
25.
Seleman Liwowa
Kilindi
26.
Josephine R. Matiro
Makete
27.
Gerald J. Guninita
Kilolo
28.
Senyi S. Ngaga
Mbinga
29.
Mary Tesha
Ukerewe
30.
Rodrick Mpogolo
Chato
31.
Christopher Magala
Newala
32.
Paza T. Mwamlima
Mpanda
33.
Richard Mbeho
Biharamulo
34.
Jacqueline Liana
Magu
35.
Joshua Mirumbe
Bunda
36.
Constantine J.  Kanyasu
Ngara
37.
Yahya E. Nawanda
Iramba
38.
Ulega H. Abadallah
Kilwa
39.
Paul Mzindakaya
Busega (mpya)
40.
Festo Kiswaga
Nanyumbu
41.
Wilman Kapenjama Ndile
       Mtwara
42.
Joseph Joseph Mkirikiti
Songea
43.
Ponsiano Nyami
Tandahimba
44.
Elibariki Immanuel Kingu
Kisarawe
45.
Suleiman O. Kumchaya
Tabora
46.
Dkt. Charles O. F. Mlingwa
Siha
47.
Manju Msambya
Ikungi (mpya)
48.
Omar S. Kwaangw’
Kondoa
49.
Venance M. Mwamoto
Kibondo
50.
Benson Mpesya
Kahama
51.
Daudi Felix Ntibenda
Karatu
52.
Ramadhani A. Maneno
Kigoma
53.
Sauda S. Mtondoo
Rufiji
54.
Gulamhusein Kifu
Mbarali
55.
Esterina Kilasi
Wanging’ombe (mpya)
56.
Subira Mgalu
Muheza
57.
Martha Umbula
Kongwa
58.
Rosemary Kirigini
Meatu
59.
Agness Hokororo
Ruangwa
60.
Regina Chonjo
Nachingwea
61.
Ahmed R. Kipozi
       Bagamoyo
62.
Wilson Elisha Nkhambaku
       Kishapu
63.
Amani K. Mwenegoha
       Bukombe
64.
Hafsa M. Mtasiwa
       Pangani
65.
Rosemary Staki Senyamule
      Ileje
66.
Selemani Mzee Selemani
      Kwimba
67.
Lt. Col. Ngemela E. Lubinga
     Mlele (mpya)
68.
Iddi Kimanta
      Nkasi
69.
Muhingo Rweyemamu
     Handeni
70.
Lucy Mayenga
     Uyui