.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, December 11, 2012

CRDB yabisha hodi Burundi

Jengo la CRDB Jijini Bujumbura Burundi

Rais wa Burundi Piere Nkurunzinza  akikata utepe wa jengo la CRDB. Kulia ni Dkt Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB

Balozi wa Tanzania nchini Burundi (kushoto) akiteta neno na Dkt Kimei (kulia)

Wafanyakazi wa CRDB Burundi na Tanzania kwenye picha ya pamoja.

Bunge Sports Club netball yaongoza kwa mabao 100:


Tanzania


Tanzania Bunge Sport Club Netball imefanikiwa kuwa kileleni baada ya kuitandika timu ya muungano ya Jumuiya na Bunge la Afrika Mashariki kwa mabao 49-9. Katika mchezo mkali wa mashindao ya michezo ya mabunge yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya, timu ya Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachakaza bila huruma wenyeji wao Kenya kwa mabao 51-25. Mashindano haya ambayo huandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Bunge la Afrika Mashariki kwa lengo la kudumisha mshikamano, yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 14 Disemba 2012. Tayari Tanzania imeweka kibindoni mabao 100, mtaji ambo si rahisi kfikiwa na timu nyingine zilizosalia.

Tayari Tanzania Bunge Sports Club Football wameshajihakikishia kuingia nusu fainali  baada ya kutoa adhabu kali kwa timu za Kenya na Rwanda.  Kwenye mechi yake na Kenya, Tanzania ilijipatia mambo 5-0. Aidha kwenye mchezo wake na Rwanda Tanzania iliifunga Rwanda mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa City.

Awali Kenya Bunge Sports Club Football ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Mashariki katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanya wa Nyayo mbele ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo Zziwa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo. Aidha kwenye mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki Uganda ilijipatia mabao 2 -1, huku Rwanda ikijipatia magoli 2-0 dhidi ya Kenya.

Wakishangilia


Afrika Mashariki

Sunday, December 9, 2012

Tanzania yatisha


Kikosi cha Tanzania
 
Tanzania yaendeleza ubabe wa kwa timu za mabunge ya
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya timu ya
mpira wa kikapu wananwake kuinyanyasa Kenya Bunge
Sports Club kwa mabao 51-25. Wakati huohuo, timu ya
wanaume imeedelea kutoa adhabu kali leo ikiwa ni zamu
ya Rwanda ambapo hadi kipenga cha mwisho Tanzania 6
Rwanda 0. Jana Kenya ilibamizwa bao 5-0

 Kikosi cha Kenya

Mwanzo wa karamu ya mabao

Mlinda mlango wa Rwanda (wanaume) akinyanyasika golini

Mambo yalipokuwa magumu Rwanda (wanaume) wakamwingiza mwanamke

Saturday, December 8, 2012

Mashindano ya michezo ya Wabunge yaanza Nairobi
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth Natongo Zziwa akifungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa wabunge wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya ambayo hafanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda, Bunrundi, Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote ambao wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.


Maandamano ya uzinduzi
Kikosi cha Tanzania wakati wa uzinduzi.
 


Kikosi cha Uganda: Baada ya uzinduzi timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la
Afrika Mashariki ndizo zilizofungua dimba ambapo zilitoka sare ya bao moja
kwa moja. Mechi itakayofuata ni kati ya Tanzania na Kenya.


Kikosi cha Afrika Mashariki
 


Kikosi cha Tanzania kikiusoma mchezo kati ya Uganda na Afrika MasharikiMuamuzi wa mchezo huo Bi Damaris Kimani kutoka Kenya.

Sunday, December 2, 2012

EAC yapata jengo la Makao Makuu Arusha

Spika Makinda akimkaribisha Rais Kikwete katika uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu yaJumuiya ua  Afrika Mashariki jijini Arusha

 Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margareth Natongo Zziwa akimkaribisha Spika wa Bunge la Tanzania kwenye Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki ndani ya Jengo la Jumuiya hiyo

Spika Zziwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uzinduzi wa ukumbi wa Bunge

 Rais Kikwete akilihutubia Bunge la Afrika Mashariki
 Picha ya pamoja
Muonekano wa Jengo kwa nje

Tunao Miss Tanzania wangapi?

 Miss Tanzania Original Birigite Alfred
Miss Tanzania feki Maggie Munthali