.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, October 31, 2011

Wakati umefika wa kuwa na chuo kikuu cha wanawake Tanzania-Spika


       Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe Mwananzila akimkaribisha Spika Bunge Mhe. Anne Makinda aliposimama mkoani hapo akielekea Mtwara Masasi jana kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambayo imetiza miaka mia moja tangu ianzishwe mwaka 1911.

      Mkuu wa Shule ya wasichana Masasi Mama Tesha akimpokea Spika Makinda kwenye shule hiyo. Mhe Spika alisoma katika shule hii mwaka 1965-1968 ambapo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU Youth league.       Bweni alilikuwa akila Mhe Makinda wakati akiwa shuleni hapo

      Spika Makinda akiwa na “School mates” jana alipotembelea Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi ambapo amesema ni veme kuanza kufikiria kuanzishwa kwa Chuo kikuu cha wanawake Tanzania


       Zawadi ya kinyago alichopewa Spika kinachoashira majuku ya mwananke wa kiafrika anayehitaji kupewa nafasi

       Spika Makinda akiwasili katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambapo amekuwa mgeni rasmi katika maadhisho ya miaka mia moja tangua kuanzishwa kwake na pia mahafali ya kidato cha nne akiongozwa na Mkuu wa Shule Mama Aluna Bakari kulia

       Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Abdallah (kulia) akimfahamisha jambo mhe. Spika wakati wa ziara katika shule ya Ndwika leo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima

      Umaahiri wa ukandarasi wa awali umekwenda wapi?... haya ni majengo ya mabweni ya wanafunzi Ndwika yaliyojengwa zaidi ya miaka miamoja iliyopita


       Spika Makinda akiweka jiwe la msingi katika jingo la teknolojia ya maarifa katika sekondari ya ndwika ambako aliendesha harambee iliyokusanya shilingi 27,600,000/- ili kukamisha ujenzi

  Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyeibuka kidedea katika masomo yote, Bi Mwajuma Issa, akipongezwa na Mhe. Spika huku Menyekiti wa Bodi ya Shule Bw. Juma Satna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima na Mkuu wa wilaya za Nanyumbu na Masasi Mhe Fatma Ally wakishuhudia.

Tuesday, October 18, 2011

Tunataka mgawanyo sawa wa madaraka na siyo utajiri-IPU yauambia Umoja wa Mataifa

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda leo akichangia wakati
wa mjadala kuhusu fedha na mdororo wa uchumi duniani ambapo amezitaka
nchi zilizoendelea kutojisahau kwa kudhani kuwa maendeleo ya nchi hizo
 hayana uhusiano wa moja kwa moja na nchi zinazoendelea. Hivyo mataifa
yote yanahitaji kuungana na kufanyakazi pamoja. Kulia kwake ni Kamishna
wa Bunge Mhe. Hamadi Rashid Hamadi ambaye alihudhuria kikao hicho.

Makamu wa Rais wa Kamati ya Bunge la Dunia inayoshughulikia
maendeleo endelevu, Fedha na Biashara Mhe. Hamad Rashid Hamad
ametaka Umoja wa Mataifa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha mataifa
machanga cha kupata uwaklishi ulio sawa katika vyombo vya kutoa
maamuzi hasa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vyombo
vya fedha (IFM,WB) na kuongeza uwazi katika chombo cha kimataifa cha
Biashara (WTO) ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikiwatajirisha
matajiri na kuwaumiza wazalishaji wan chi maskini. Mhe Hamadi (kati)
akiwa na Mhe. Susan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki amesema kinachotakiwa
ni mgawanyo wa madaraka na siyo wa utajiri tu.

Mhe. Suzan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki wakifuatilia majadiliano
ya wajibu wa wabunge wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora
ya afya kwa wanawake na watoto ambapo ujumbe wa Tanzania
ulielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kutekeleza malengo namba
nne na tano ya millennia ikiwa ni pamoja na changamoto zake.


Kaimu Katibu wa Bunge Bw. John Joel akishauriana na Katibu wa
msafara Bw. James Warburg kwenye kikao cha Chama cha Makatibu
wa mabunge  wa IPU kabla ya uchuguzi wa Rais wa Chama hicho leo.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdulrahmin Abdi akihutubia Baraza Kuu la IPU na kuitaka dunia iisadie Somali badala ya kuichia Afrika Mashariki peke yake.


Viongozi mbalimbali wakiifuatilia hotuba ya Mhe. Abdi kwa makini


Spika Makinda na Mhe. Hamadi wakibadilishana mawazo na mmoja wa mjumbe wa IPU


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Masha Fortunatus afuatilia mjadala

Uganda ndiyo itakayoandaa mkutando wa IPU Marchi 2012. Haya ni baadhi tu ya maandalizi ambao wameanza kufanya kwa ajili ya mkutano huo. Vyombo vya muziki wa utamaduni.

Ni wakati wa Dunia kubadilika na kuwapa wanawake nafasi zaidi, IPU yaambiwa. Afrika Mashariki yapongezwa

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akijadilana jambo na Mhe. Angella Kairuki Mb, mara kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza Kuu la IPU leo ambapo suala la wanawake kupewa nafasi limejitokeza kwa nguvu kubwa, huku Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) ikipongezwa kwa kuwa na maspika watatu wanawake kati ya watano. Aidha Rwanda imekuwa kinara kwa kuwa na 56% ya wabunge wanawake.

Viongozi mbalimbali wa mabunge duniani wakishiriki katika kikao hicho ambapo kitabu cha ushiriki wa watoto katika Bunge “Child Participation in Parliament) na chapisho la Gender- Sensitive Parliaments: A Global Review of Good Practice” vilizinduliwa rasmi leo.

Kaimu Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel (katikati) na watendaji waandamizi wa Ofisi ya Bunge Bw. D.Eliufoo (kulia) na Bw. J. Warburg (kushoto) wakifuatilia mwenendo wa kikao leo.

Mhe. Angeala Kairuki na Mhe. Spika Makinda wakati wa kikao

Kiongozi-mwenza wa kupiga vita matumizi mabaya ya Nuclear na silaha Dkt Raphael Chegen akiendasha kikao cha Nuclear Non-Proliferation and Disarmament katika mkutano wa 125 wa IPU.

Mhe. Susan Lyimo wa Tanzania na Mhe. Fortunatus Masha wa Bunge la Afrika Mashariki ni wajumbe wa  kamati ya Nuclear Non Proliferation and Disarmament ya Inter-Parliamentary Union –IPUMhe. Masha FortunatusSpika wa Bunge la Uganda Mhe Rebecca Kadaga akielezea mafanikio ya Afrika Mashariki katika kuwapa wanawake nafasi

Kaimu Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel (kati) akitoa maelekezo kwa Afisa Itifaki wa IPU


Katibu Mkuu wa CPA Dkt. William Shija


Sunday, October 16, 2011

Wabunge warudishieni imani wananchi: Ban-Ki Moon

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda yuko nchini Uswissi kuhudhuria Mkutano wa 125 wa  Chama cha Muungano wa Mabunge Ulimwenguni (Interparliamentary Union-IPU). Hapa akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani/Uswissi Balozi A. Ngemera mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano leo jioni.


Balozi Ngemera akimpa Mhe. Spika muhtasari wa mkutano

Katibu Mkuu wa Chama cha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association-CPA) Dkt William Shija akizungumza na Spika Makinda.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  125 wa IPU katika mji wa Bern. Hotuba yake iliyowavuta wengi ilihusu changamoto zinazoikabili dunia ya leo: “siyo upungufu wa bajeti bali ni upungufu wa imani kwa serikali na taasisi mbalimbali”.

Spika Makinda na Spika  wa Bunge la Uganga Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga wakiifuatilia hotuba hiyo kwa umakini mkubwa

Maspika, Wabunge, Makatibu wa Bunge, Maafisa na watendaji mbalimbali katika mabunge duniani wakifuatilia hotuba za ufunguzi: Dkt. Williama Shija

Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge Mhe. Hamad Rashid na aliyekuwa Mbunge wa Busega Dkt. Chegeni

Ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania: Mhe. Susan Lyimo, Dkt Chegeni (mbunge wa zamani), Mhe. Hamad Rashid na Angela Kairuki


MHE. David Kafulila akiwa kwenye mkutano wa IPU na mbunge rafiki yake kutoka Canada


Muwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel na katibu wa msafara Bw. James Warburg


Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Abdirahin Abdi.

Picha ya pamoja ya Spika wa Bunge, Balozi Ngemera na ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania

Spika na Balozi...tete-a-tete

Mtoto wa miaka mitano aonesha maajabu kwa kucheza piano kwenye mkutano wa IPU

Watu mashuhuri wakimshangaa na kumshangilia mtoto huyo

Mwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania (kati) akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Spika Makinda na Balozi Ngemera


Uganda ilituma ujumbe mkubwa kwani ndiyo waandaji wa mkutano wa IPU unaofuata


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiondoka ukumbiniMonday, October 10, 2011

Wasomi Korea waomba ubalozi


 Spika Makinda (katikati) akiwa na Bw Emmanuel Lupila
Mwenyekiti Kulia na Bw. Severini Kapinga Katibu wa
Watanzania waishio Korea.

Wakati wa kuahirisha ziara yake nchini Korea Kusini jana nioni,  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda alikutana na watanzaia wanaoishi nchini humo katika Chuo Cha Maendeleo cha Korea (KDI) ambapo waliiomba serikali kupitia kwake (Spika) kutafakari kufungua ubalozi nchini Korea Kusini kwani kuna mengi yatakayoinufaisha Tanzania.  Tayari nchi jirani ya Kenya imefungua ubalozi nchini Korea.
Watanzania hao wapatao sitini ambao wengi wao ni wanafunzi wa elimu ya juu walitanabaisha kuwa Korea Kusini ni nchi ambayo ilikuwa maskini sana miaka michache iliyopita lakini imefanya mapinduzi ya kiuchumi na sasa ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea duniani. “Ni bora kujifunza kutoka kwenye nchi zinazokuwa kwa kasi tukiziona kuliko kutegemea nchi zilizoendelea zamani kama vile za ulaya na Marekani” alisema Bw. Lwenje ambaye ni mwanafunzi wa shada ya uzamili ya uchumi. Katika risala yao, wameiomba  serikali pia itumie vizuri fursa za masomo  zilizopo nchini Korea kwa kupeleka wanafunzi wengi zaidi kwa manufaa ya nchi. Aidha waliiomba serika iharakishe mpango wa kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwani ni jambo ambalo kwa sasa hivi halikwepeki tena.
Mhe. Spika akiwaahidi kuyafikisha maombi yao serikalini amewataka kudumisha nidhamu, kufanyakazi kwa bidii na kudumisha uzalendo wa nchi yao. “Ninyi ndiyo chachu na wakala wa mageuzi mara mtakapomaliza masomo yenu na kurejea nyumbani mkiwa na utaalamu na uzoefu wa yale mtakayokuwa mmejifunza huku” aliwaasa Mhe. Makinda. Aliwahamisha kuwa hali ya numbani ni shwari ila changamoto ni nyingi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwamba jitihada kubwa zinafanyika kuondoa tatizo la umeme na mchakato wa katiba mpya unaendelea.

 Bw. Lwenje akifafanua jambo

   Kipindi cha maswali na ufafanuzi


Mtanzania aishiye Korea Kusini Mtoto Faith Sanga akitoa zawadi kwa Mhe. Spika kwa niaba ya kundi zima

   Mwendesha shughuli Bi Juliana Masawe (kushoto) akimpongeza Faith na kumshukuru Mhe. Spika kwa kuja kuonana nao


   Picha ya pamoja