.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, August 29, 2012

Ujumbe wa Tz wapata somo la mkutano wa Makazi

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa ofisini kwake leo na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Goodluck Ole Medeye. Mhe Medeye alikuja kumpa Mhe Spika muhtasari wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi utakaofanyika Napole, Italia kuanzia tarehe 1 hadi 6 Septemba 2012 ambapo Spika makinda na maspika wengine kutoka bara la Afrika wamealikwa kushiriki.
Mhe. Ole Medeye akiutanbulisha ujumbe wa Tanzania utakaohudhuria mkutano huo. Ujumbe huu unahusisha taasisi mbalimbali kama vile Halmashauri, Sumatra, Wasafirishaji, wataalamu wa Ardhi na wataalamu wa Makazi


Spika Makinda akiuasa ujumbe huo kuhudhuria mkutano huo kwa lengo la kuikwamua na kuivusha Tanzania kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Kuimarisha Muungano wa Tanzania

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hammad Mussa akisalimiana na rafiki yake, Mhe. James Mbatia walipokutana mjini Dodoma hivi karibuni. Mhe Muss aliongoza ujumbe wa watu watano kuhudhuria mkutano wa chama cha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania kilichofanyika mjini Dodoma
Wajumbe wakisaliana na mwenyekiti huyo.






Maafisa wa Bunge  (Prosper Minja-kulia na Nuru Venance - kati) wakimsikiliza mmoja wa wawakilishi kutoka Zanzibar (kushoto)





20 BORA WA KIDATO CHA SITA 2012



Friday, August 24, 2012

Dar is changing .... Positive change?

Tegeta


Mikocheni


Msasani

Michezo huyapa mahusiano ya kidiplomasia afya njema!

Rais wa Jamhuri ya Rwanda Paul Kagame akisalimiana na Vingozi na Timu nzima ya Washindi wa Kombe la Kagame, Yanga, walipomtembnelea Ofisini kwake kufuatia mwaliko alioutoa kwa timu hiyo. Michezo zaidi ya kujenga urafiki inaimarisha diplomasia ya nchi moja na nyingine,

Thursday, August 16, 2012

TASSAF Awamu nyingine

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda (kushoto) wakati wa kukagua miradi ya TASSAF jana mjini Dodoma

Wednesday, August 15, 2012

BUPAT wafundwa, Wanafunzi bora wazawadiwa

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwafunda wanachama  wa Chama wa chama cha Waandishi wa habari za BUnge (BUPAT)jinsi ya kuandika habari za Bunge kwa kutofautisha ni zipi habari za Bunge na ni zipi habari za ofisi ya Bunge na pia ni zipi habari za mbunge mmoja mmoja  mjini Dodoma hivi karibuni. Kulia kwake ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Ayub Ryoba na mtoa mada katika semina hiyo.


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mkuu wa Freemedia Bw. Absalom Kibanda
akitoa mada kwenye semina hiyo


Wadau wakifuatilia mijadala



Dkt Ryoba


Wadau



Restuta James

Florian Kaijage

Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Ofisi ya Bunge
 Bw. Jossey Mwakasyuka akihitimisha mjadala


Waliofauluri kidato cha sita 2012 walizawadiwa na Waziri Mkuu baada ya kukuribishwa rasmi Bungeni

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwatambulisha Bungeni wanafunzi 20 waliofaulu vizuri mitihani ya Kidato cha sita 2011


Wahitimu hao wakiwa kwenye picha ya pamoja. Hapa wapo na Mbunge wa Mafia Mhe, A. Shah (mwenye tai nyekundu)  Mh. Agnes Hokororo, (kulia kwa Mhe. Shah) Mhe. neema Mgaya(wa kwanza kushoto)  na Mhe. Kabati (kulia)












Friday, August 10, 2012

Spika Makinda akutana na Tume ya Huduma za Bunge la Malawi

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) kwa pamoja wakiwa na mazungumzo ya kina leo na ujumbe wa Tume ya Huduma za Bunge la Malawi ulioko nchini hivi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia uhusiano mzuri wa mabunge ya nchi mbili hizi. Kushoto kwa Mhe. Ndugai ni Naibu Spika wa Bunge la Malawi Mhe.Juliana Mpande (Mb) ambaye ni mkuu wa msafara. Wengine ni Kamishna Alfred Mwechumu (Mb) na Kamishna Christina Chiwowo (Mb).


Spika wa Bunge la Tanzania akiwa na mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofika ofisini kwake Dodoma leo. Spika Makinda amewataka na kuwaasa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.
Picha na Prosper Minja - Bunge

Thursday, August 9, 2012

Prof Mahalu na wenzake waibuka kidedea!

Prof Costa Mahalu (wa pili kushoto) na Bi Grace Martin wa kwanza kushoto wakizungumza na waandishi wa Habari baada ya mahakama kutowatia hatiani kufuatia kesi ya ununuaji wa jengo la Ubalozi Roma Italia.

Monday, August 6, 2012

Dkt Migiro awafunda wanawake wabunge wa Tanzania

Spika Makinda na mgeni wake ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Umija wa Mataifa aliyemaliza muda wake Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na wabunge wanawake wa Tanzania. Dkt Migiro yuko Dodoma kwa mwaliko wa Spika wa Bunge. Awapa siri ya mafanikio yake. Awataka kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Mdau alipata fursa ya kukuta na Nyota hii ya Afrika


Dkt Migiro (katikati) Bi Theddy Ladislaus (kulia) na Bw. Herman Berege

Spika Makinda na wadau

Futar