.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, August 29, 2012

Ujumbe wa Tz wapata somo la mkutano wa Makazi

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa ofisini kwake leo na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Goodluck Ole Medeye. Mhe Medeye alikuja kumpa Mhe Spika muhtasari wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi utakaofanyika Napole, Italia kuanzia tarehe 1 hadi 6 Septemba 2012 ambapo Spika makinda na maspika wengine kutoka bara la Afrika wamealikwa kushiriki.
Mhe. Ole Medeye akiutanbulisha ujumbe wa Tanzania utakaohudhuria mkutano huo. Ujumbe huu unahusisha taasisi mbalimbali kama vile Halmashauri, Sumatra, Wasafirishaji, wataalamu wa Ardhi na wataalamu wa Makazi


Spika Makinda akiuasa ujumbe huo kuhudhuria mkutano huo kwa lengo la kuikwamua na kuivusha Tanzania kutoka hatua moja kwenda nyingine.