.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, October 18, 2011

Tunataka mgawanyo sawa wa madaraka na siyo utajiri-IPU yauambia Umoja wa Mataifa

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda leo akichangia wakati
wa mjadala kuhusu fedha na mdororo wa uchumi duniani ambapo amezitaka
nchi zilizoendelea kutojisahau kwa kudhani kuwa maendeleo ya nchi hizo
 hayana uhusiano wa moja kwa moja na nchi zinazoendelea. Hivyo mataifa
yote yanahitaji kuungana na kufanyakazi pamoja. Kulia kwake ni Kamishna
wa Bunge Mhe. Hamadi Rashid Hamadi ambaye alihudhuria kikao hicho.

Makamu wa Rais wa Kamati ya Bunge la Dunia inayoshughulikia
maendeleo endelevu, Fedha na Biashara Mhe. Hamad Rashid Hamad
ametaka Umoja wa Mataifa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha mataifa
machanga cha kupata uwaklishi ulio sawa katika vyombo vya kutoa
maamuzi hasa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vyombo
vya fedha (IFM,WB) na kuongeza uwazi katika chombo cha kimataifa cha
Biashara (WTO) ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikiwatajirisha
matajiri na kuwaumiza wazalishaji wan chi maskini. Mhe Hamadi (kati)
akiwa na Mhe. Susan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki amesema kinachotakiwa
ni mgawanyo wa madaraka na siyo wa utajiri tu.

Mhe. Suzan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki wakifuatilia majadiliano
ya wajibu wa wabunge wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora
ya afya kwa wanawake na watoto ambapo ujumbe wa Tanzania
ulielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kutekeleza malengo namba
nne na tano ya millennia ikiwa ni pamoja na changamoto zake.


Kaimu Katibu wa Bunge Bw. John Joel akishauriana na Katibu wa
msafara Bw. James Warburg kwenye kikao cha Chama cha Makatibu
wa mabunge  wa IPU kabla ya uchuguzi wa Rais wa Chama hicho leo.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdulrahmin Abdi akihutubia Baraza Kuu la IPU na kuitaka dunia iisadie Somali badala ya kuichia Afrika Mashariki peke yake.


Viongozi mbalimbali wakiifuatilia hotuba ya Mhe. Abdi kwa makini


Spika Makinda na Mhe. Hamadi wakibadilishana mawazo na mmoja wa mjumbe wa IPU


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Masha Fortunatus afuatilia mjadala

Uganda ndiyo itakayoandaa mkutando wa IPU Marchi 2012. Haya ni baadhi tu ya maandalizi ambao wameanza kufanya kwa ajili ya mkutano huo. Vyombo vya muziki wa utamaduni.