.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, October 31, 2011

Wakati umefika wa kuwa na chuo kikuu cha wanawake Tanzania-Spika


       Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe Mwananzila akimkaribisha Spika Bunge Mhe. Anne Makinda aliposimama mkoani hapo akielekea Mtwara Masasi jana kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambayo imetiza miaka mia moja tangu ianzishwe mwaka 1911.

      Mkuu wa Shule ya wasichana Masasi Mama Tesha akimpokea Spika Makinda kwenye shule hiyo. Mhe Spika alisoma katika shule hii mwaka 1965-1968 ambapo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU Youth league.



       Bweni alilikuwa akila Mhe Makinda wakati akiwa shuleni hapo

      Spika Makinda akiwa na “School mates” jana alipotembelea Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi ambapo amesema ni veme kuanza kufikiria kuanzishwa kwa Chuo kikuu cha wanawake Tanzania


       Zawadi ya kinyago alichopewa Spika kinachoashira majuku ya mwananke wa kiafrika anayehitaji kupewa nafasi

       Spika Makinda akiwasili katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambapo amekuwa mgeni rasmi katika maadhisho ya miaka mia moja tangua kuanzishwa kwake na pia mahafali ya kidato cha nne akiongozwa na Mkuu wa Shule Mama Aluna Bakari kulia

       Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Abdallah (kulia) akimfahamisha jambo mhe. Spika wakati wa ziara katika shule ya Ndwika leo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima

      Umaahiri wa ukandarasi wa awali umekwenda wapi?... haya ni majengo ya mabweni ya wanafunzi Ndwika yaliyojengwa zaidi ya miaka miamoja iliyopita


       Spika Makinda akiweka jiwe la msingi katika jingo la teknolojia ya maarifa katika sekondari ya ndwika ambako aliendesha harambee iliyokusanya shilingi 27,600,000/- ili kukamisha ujenzi

  Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyeibuka kidedea katika masomo yote, Bi Mwajuma Issa, akipongezwa na Mhe. Spika huku Menyekiti wa Bodi ya Shule Bw. Juma Satna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima na Mkuu wa wilaya za Nanyumbu na Masasi Mhe Fatma Ally wakishuhudia.