.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Sunday, October 16, 2011

Wabunge warudishieni imani wananchi: Ban-Ki Moon

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda yuko nchini Uswissi kuhudhuria Mkutano wa 125 wa  Chama cha Muungano wa Mabunge Ulimwenguni (Interparliamentary Union-IPU). Hapa akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani/Uswissi Balozi A. Ngemera mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano leo jioni.


Balozi Ngemera akimpa Mhe. Spika muhtasari wa mkutano

Katibu Mkuu wa Chama cha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association-CPA) Dkt William Shija akizungumza na Spika Makinda.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  125 wa IPU katika mji wa Bern. Hotuba yake iliyowavuta wengi ilihusu changamoto zinazoikabili dunia ya leo: “siyo upungufu wa bajeti bali ni upungufu wa imani kwa serikali na taasisi mbalimbali”.

Spika Makinda na Spika  wa Bunge la Uganga Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga wakiifuatilia hotuba hiyo kwa umakini mkubwa

Maspika, Wabunge, Makatibu wa Bunge, Maafisa na watendaji mbalimbali katika mabunge duniani wakifuatilia hotuba za ufunguzi: Dkt. Williama Shija

Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge Mhe. Hamad Rashid na aliyekuwa Mbunge wa Busega Dkt. Chegeni

Ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania: Mhe. Susan Lyimo, Dkt Chegeni (mbunge wa zamani), Mhe. Hamad Rashid na Angela Kairuki


MHE. David Kafulila akiwa kwenye mkutano wa IPU na mbunge rafiki yake kutoka Canada


Muwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel na katibu wa msafara Bw. James Warburg


Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Abdirahin Abdi.

Picha ya pamoja ya Spika wa Bunge, Balozi Ngemera na ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania

Spika na Balozi...tete-a-tete

Mtoto wa miaka mitano aonesha maajabu kwa kucheza piano kwenye mkutano wa IPU

Watu mashuhuri wakimshangaa na kumshangilia mtoto huyo

Mwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania (kati) akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Spika Makinda na Balozi Ngemera


Uganda ilituma ujumbe mkubwa kwani ndiyo waandaji wa mkutano wa IPU unaofuata


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiondoka ukumbini