.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, October 18, 2011

Ni wakati wa Dunia kubadilika na kuwapa wanawake nafasi zaidi, IPU yaambiwa. Afrika Mashariki yapongezwa

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akijadilana jambo na Mhe. Angella Kairuki Mb, mara kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza Kuu la IPU leo ambapo suala la wanawake kupewa nafasi limejitokeza kwa nguvu kubwa, huku Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) ikipongezwa kwa kuwa na maspika watatu wanawake kati ya watano. Aidha Rwanda imekuwa kinara kwa kuwa na 56% ya wabunge wanawake.

Viongozi mbalimbali wa mabunge duniani wakishiriki katika kikao hicho ambapo kitabu cha ushiriki wa watoto katika Bunge “Child Participation in Parliament) na chapisho la Gender- Sensitive Parliaments: A Global Review of Good Practice” vilizinduliwa rasmi leo.

Kaimu Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel (katikati) na watendaji waandamizi wa Ofisi ya Bunge Bw. D.Eliufoo (kulia) na Bw. J. Warburg (kushoto) wakifuatilia mwenendo wa kikao leo.

Mhe. Angeala Kairuki na Mhe. Spika Makinda wakati wa kikao

Kiongozi-mwenza wa kupiga vita matumizi mabaya ya Nuclear na silaha Dkt Raphael Chegen akiendasha kikao cha Nuclear Non-Proliferation and Disarmament katika mkutano wa 125 wa IPU.

Mhe. Susan Lyimo wa Tanzania na Mhe. Fortunatus Masha wa Bunge la Afrika Mashariki ni wajumbe wa  kamati ya Nuclear Non Proliferation and Disarmament ya Inter-Parliamentary Union –IPU



Mhe. Masha Fortunatus



Spika wa Bunge la Uganda Mhe Rebecca Kadaga akielezea mafanikio ya Afrika Mashariki katika kuwapa wanawake nafasi

Kaimu Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel (kati) akitoa maelekezo kwa Afisa Itifaki wa IPU


Katibu Mkuu wa CPA Dkt. William Shija