JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE
LA TANZANIA
TAARIFA
KWA UMMA
YAH:
MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015
_______________
1.0
UTANGULIZI
Mkutano wa
Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12
Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha
Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa
na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.
Hivyo, Wabunge
wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria
kikao cha briefing siku ya Jumatatu
tarehe 11 Mei, 2015.
2.0
SHUGHULI
ZITAKAZOTEKELEZWA
Katika Mkutano
huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa
majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri Mkuu na
kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.
Aidha, katika
mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya
mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu
hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa
Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.
Baada ya hayo,
Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa mwaka
wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa
Fedha 2015/2016.
Siku ya Alhamisi
tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne) asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha
taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali
kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.
Mjadala wa hotuba
ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na
kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili
na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.
3.0 SHUGHULI
NYINGINE
Shughuli za Mkutano
wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba
ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.
Ratiba kamili ya
shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti ya
Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM
08 Mei 2015
RATIBA YA MKUTANO WA
BUNGE LA BAJETI, KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016 TAREHE 12 MEI, 2015 HADI
27 JUNI, 2015
NA.
|
TAREHE NA
SIKU
|
SHUGHULI HUSIKA NA WIZARA
|
1.
|
JUMAMOSI
na
JUMAPILI
09/05/2015 -10/05/2015
|
Wabunge
kuelekea Dodoma kutoka Dar es Salaam na sehemu mbalimbali.
|
2.
|
JUMATATU
11/05/2015
Saa 4.00 Asubuhi
Saa 10.00 Jioni
|
· Kikao cha Pamoja cha
Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti (Ukumbi wa Pius Msekwa)
·
Kikao cha Briefing kwa Wabunge wote
(Ukumbi wa Pius Msekwa)
|
3.
|
JUMANNE - JUMAMOSI
12/5/2015 - 16/5/2015
|
Mkutano wa Bunge kuanza
kwa shughuli zifuatazo.
(i)
Maswali ;
HOTUBA YA BAJETI YA OFISI
YA WAZIRI MKUU: (Siku 5)
·
SERA, URATIBU
NA BUNGE.
·
UWEKEZAJI NA
UWEZESHAJI.
·
TAWALA ZA
MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
|
4.
|
JUMATATU
18/5/2015
|
HOTUBA YA BAJETI YA OFISI
YA RAIS:
- MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
|
5.
|
JUMANNE
19/5/2015
|
HOTUBA YA BAJETI YA OFISI
YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA).
|
6.
|
JUMATANO
20/5/2015
|
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
|
7.
|
ALHAMISI
21/5/2015
|
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA KATIBA NA SHERIA
|
8.
|
IJUMAA
22/5/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
|
9.
|
JUMAMOSI
23/5/2015
|
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
|
10.
|
JUMATATU
25/5/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA.
|
11.
|
JUMANNE
26/5/2015
|
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
|
12.
|
JUMATANO
27/5/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA UJENZI
|
13.
|
ALHAMISI
28/5/2015
|
·
Maswali
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA
UTALII.
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
|
14.
|
IJUMAA
29/5/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI.
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA.
|
15.
|
JUMAMOSI
30/5/2015
|
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA UCHUKUZI
|
16.
|
JUMATATU
01/6/2015
|
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA UFUNDI
|
17.
|
JUMANNE
02/6/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
|
18.
|
JUMATANO
03/6/2015
|
·
Maswali
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAJI.
|
19.
|
ALHAMISI
04/6/2015
|
·
Maswali
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
|
20.
|
IJUMAA
05/6/2015
|
·
Maswali.
·
HOTUBA YA
BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.
|
21
|
JUMAMOSI
06/06/2015
|
- HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA
|
22.
|
JUMATATU - JUMATANO
08/6/2015 – 10/6/2015
|
Serikali
kushauriana na Kamati ya Bajeti Kufanya Majumuisho kuzingatia Hoja
zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara;(Siku 3)
|
23.
|
ALHAMISI
11/6/2015
|
·
Maswali
(i)
Waziri
anayehusika na Mipango Kusoma Taarifa ya Hali ya Uchumi.
(ii)
Waziri wa
Fedha Kusoma Hotuba ya Bajeti ya Serikali.
|
24.
|
IJUMAA
12/6/2015
|
Wajumbe Kusoma na kutafakari Hotuba ya Bajeti.
|
25.
|
JUMATATU - JUMANNE
15/6/2015 - 23/6/2015
|
·
Maswali
·
MJADALA KUHUSU
BAJETI YA SERIKALI
(Siku 7)
|
26.
|
JUMATANO
24/6/2015
|
·
Maswali
·
Muswada wa
Sheria ya Fedha za Matumizi (The
Appropriation Bill, 2015)
·
Muswada wa
Sheria ya Fedha (The Finance Bill,
2015)
|
27.
|
ALHAMISI - IJUMAA
25/6 – 26/6/2015
|
·
Maswali
·
Muswada wa
Sheria ya Fedha (The Finance Bill,
2015)
|
28.
|
JUMAMOSI
27/6/2015
|
KUFUNGA BUNGE
|