.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, May 11, 2015

Mkutano wa Bunge, Ratiba


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA
YAH: MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015
_______________


1.0       UTANGULIZI
Mkutano wa Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12 Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.

Hivyo, Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma  ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria kikao cha briefing siku  ya Jumatatu tarehe 11 Mei, 2015.

2.0       SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
Katika Mkutano huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri Mkuu na kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya  Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.

Aidha, katika mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Baada ya hayo, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.

Siku ya Alhamisi tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne)  asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.

Mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.

3.0 SHUGHULI NYINGINE
Shughuli za Mkutano wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.

Ratiba kamili ya shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM
08  Mei 2015

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE LA BAJETI, KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016 TAREHE 12 MEI, 2015 HADI
27 JUNI, 2015

NA.
TAREHE NA SIKU

SHUGHULI HUSIKA NA WIZARA
1.
JUMAMOSI
na
JUMAPILI
09/05/2015 -10/05/2015
Wabunge kuelekea Dodoma kutoka Dar es Salaam na sehemu mbalimbali.
2.
JUMATATU
11/05/2015

Saa 4.00 Asubuhi


Saa 10.00 Jioni


·    Kikao cha Pamoja cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti (Ukumbi wa Pius Msekwa)

·    Kikao cha Briefing kwa Wabunge wote
(Ukumbi wa Pius Msekwa)
3.
JUMANNE - JUMAMOSI
12/5/2015 - 16/5/2015
Mkutano wa Bunge kuanza kwa shughuli zifuatazo.

(i)          Maswali ;

HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU: (Siku 5)
·      SERA, URATIBU NA BUNGE.

·      UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI.

·      TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
4.
JUMATATU
18/5/2015
 • Maswali

HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA RAIS:

 • MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

 • UTAWALA BORA

 • MAHUSIANO NA URATIBU

5.
JUMANNE
19/5/2015

 • Maswali

HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA).
6.
JUMATANO
20/5/2015
 • Maswali

 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

7.

ALHAMISI
21/5/2015
 • Maswali

 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA KATIBA NA SHERIA
8.
IJUMAA
22/5/2015


·    Maswali

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
9.
JUMAMOSI
23/5/2015
 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
10.

JUMATATU
25/5/2015
·    Maswali

·  HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA.
11.
JUMANNE
26/5/2015
 • Maswali

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
12.
JUMATANO
27/5/2015
·    Maswali

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI
13.
ALHAMISI
28/5/2015
·    Maswali

 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

14.
IJUMAA
29/5/2015
·    Maswali

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI.

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA.
15.
JUMAMOSI
30/5/2015
·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UCHUKUZI
16.
JUMATATU
 01/6/2015
 • Maswali

 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
17.
JUMANNE
02/6/2015


·    Maswali

·    HOTUBA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
18.
JUMATANO
03/6/2015
·    Maswali

 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAJI.
19.
ALHAMISI
04/6/2015

·    Maswali

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
20.
IJUMAA
05/6/2015
·    Maswali.

·    HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.
21
JUMAMOSI
06/06/2015
 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA
22.
          JUMATATU  - JUMATANO
08/6/2015 – 10/6/2015
 • Maswali;

Serikali  kushauriana na Kamati ya Bajeti Kufanya Majumuisho kuzingatia Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara;(Siku 3)
23.
ALHAMISI
11/6/2015
·         Maswali

(i)             Waziri anayehusika na Mipango Kusoma Taarifa ya Hali ya Uchumi.

(ii)           Waziri wa Fedha Kusoma Hotuba ya Bajeti ya Serikali.

24.
IJUMAA
12/6/2015
Wajumbe Kusoma na kutafakari Hotuba ya Bajeti.
25.
JUMATATU - JUMANNE
15/6/2015 - 23/6/2015


·      Maswali

·      MJADALA KUHUSU BAJETI  YA SERIKALI
(Siku 7)
26.
JUMATANO
24/6/2015
·    Maswali

·    Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi (The Appropriation Bill, 2015)
·    Muswada wa Sheria ya Fedha (The Finance Bill, 2015)
27.
ALHAMISI - IJUMAA
25/6 – 26/6/2015

·    Maswali
·    Muswada wa Sheria ya Fedha (The Finance Bill, 2015)
28.
JUMAMOSI
27/6/2015

             KUFUNGA BUNGE