.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, May 12, 2015

Politik in cross-road?


Picha nzima ilikuwa hivi ,

Mbunge Agustino Mrema alialikwa na kanisa la Kinjili La Kilutheli Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya aliyekuwa askofu wa kwanza wa Kanisa hilo Stephano Moshi,mualiko ambao pia alipewa James Mbatia.

Wawili hawa bila kujua kama watakutana,Mrema ndiye aliwasili wa kwanza katika Usharika wa Kotela ambako zimefanyika sherehe hizo akiwa na gari lake na baadae aliwasili Mbatia ambaye yeye alikuwa na msafara wa magari mawili moja wapo likiwa limebeba wasaidizi wake ambalo lilikuwa na bendera kubwa ya chaa chake cha NCCR.

Moja kwa moja Mbatia alielekea katika eneo ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kupta kifungua kinywa ambako tayari Mrema alikuwa amekwisha wasili na kila mmoja kuketi maeneo tofauti.

Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa ,ghafla liliwasili Coster ikiwa imepakwa rangi ya TLP na Bendera za chama hicho na kupaki ,hii nadhani wapambe wa mrema waliamua kufanya hivyo baada ya kuna tayari Mbatia kafika kanisani hapo huku gari lake likiwa na bendera kubwa.

Baada ya kupata chai waiwli hao walisaimiana na kuanza kuzungumzo bahati mbaya walizungumza kwa lugha ya nyumbani wote wawili hivyo ilikuwa ni vigumu kufahamu mara moja nini walikuwa wakizungumza.

·  Ibada ilianza na baadae Baba Askofu Dkt Fredrick Shookatika hotuba yake alionya wasaka uongozi kujipima kabla ya kuja kwa wananchi kuwaomba ridhaa huku akitaka waeleze nini wamefanya katika kuleta maendeleo ya taifa huku akitolea mfano katika sekta ya elimu ambayo alidai miaka50 ya uhuru bado mwanafunzi wa Tanzania anakaa chini huku tukingojea msaada toka kwa wafadhili ndio watoe fedha za madawati.

Baada ya hotuba hiyo ikafika kwa wakati wa kuwaalika wageni kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshi huku wa kwanza akiwa ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,Dkt Mrema ambaye alifika mbele na kupeana mkono na baba askofu kisha akamwita mkewe Rose Mrema na kutoa kiasi cha sh laki tano.

Aliyefuatia alikuwa ni Mbunge Mbatia ambaye kabla ya kuchangia alianza kwa kusema kuwa yeye katika maswala ya elimu yeye amekwisha toa kiasi cha sh Milioni 10 kwa ajili ya shule ya sekondari ya kumbukumbu Stephano Moshi huku akihadi kutoa kiasi cha sh mil 2 kwa ajili ya taasisi hiyo hali iliyozua shangwe kubwa toka kwa waumini.

Hali hiyo ilionekana kumvuruga Mrema ambaye alilazimika kumoba msaidizi wa askofu kupatiwa nafasi ya kuzungumza kwa kuwa yeye ndiye mbunge mwenyeji ambapo alipewa na kuanza kuzungumzia maswala ya mahakama ya kadhi hali iliyozua minong'ono miongoni mwa waumini.

baadae Mrema alionekana kutoka nje huku akisindikizwa na mkewe na baadae alielekea kwenye gari lake kabla ya kumalizika kwa shughuli za ibada hiyo na kuamua kuondoka kwa kile kilichodaiwa kutojisikia vizuri.

wakati shughuli za ibada hiyo zikiendelea Mbatia alipata nafasi ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya Akofu Moshi na baadae kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Moshi.

wakiwa katika eneo la chakula ,baba askofu Dkt Shoo alimkabidhi ,mbatia Ndafu huku akisema kuwa wameamua kukabidhi chakula hicho ili kumpa nguvu katika mapambano yake katika kusaidia maendeleo ya nchi hususani katika swala la elimu.