Hatimaye
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete leo
amekalisha uteuzi wa wabunge kwa mujibu wa ibara ya 66 kifungu (1) aya ya (e)
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayompa
mamlaka ya kuteua watu wasiozidi kumi (10) kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano. Katika uteuzi huu Rais amemteua Dkt. Grace Puja na Ndugu Innocent
Sebba kuwa wabunge na tayari Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Semamba
Makinda (Mb) amewaapisha ili waweze kuanza kazi rasmi.
Wabunge
walioteuliwa na Rais kwenye Bunge la Kumi kwa mujibu wa Katiba ni wafuatao:
1.
Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhango
2.
Mhe. Dkt. Asha-Rose M. Migiro
3.
Mhe. Saada Mkuya Salum
4.
Mhe. James Francis Mbatia
5.
Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
6.
Mhe. Janet Zebedayo Mbene
7.
Mhe. Zakia Hamdani Meghji
8.
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
9.
Mhe Dkt. Grace Khwaya Puja na
10. Mhe.
Innocent Rwabushaija Sebba
Kwa
uteuzi huu idadi ya wabunge imetimia 357 kikatiba
![]() |
Mteule Innocent Sebba akila kiapo cha utii |
Spika Makinda akikabidhi vitendea kazi kwa Mbunge mteule Innocent Sebba. Anayeshuhudia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashillilah |