JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
29/03/2015
WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI
KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA
HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula
njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye
amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa
tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida
walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona
mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao
hivyo waliwakatalia kuingia.
Kundi hilo la watu 15 lilijaribu
kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini
walikamatwa na kikosi maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa
wanafuatilia mwenendo wa kundi hilo.

Silaha ambayo ni Bastola aina ya
BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA
JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya
PUMAChaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni
kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi
Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji,
Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi,
Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa
Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24,
Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi
Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri
UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62,
Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30,
Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva,
Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24,
Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60,
Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa
magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39,
Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa
kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata
uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa
madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote
zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias
Gwajima.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM