.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, November 4, 2014

Harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu zapamba moto.

Ben Komba/Pwani.

Harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu zimepamba moto kwa baadhi ya wanasiasa kujitokeza kutoka vyama mbalimbali kwa lengo la kugombea nafasi za uongozi.

Mmoja wa wanasiasa ambao nimekutana nae ambaye amenieleza kiu yake ya kugombea kiti cha Ubunge kwa tiketi ya CCM, Ni Mwalimu mstaafu BW.ISRAEL SAZIA ambaye ni Pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha wasaidizi wa Kisheria mjini Kibaha.

BW.SAZIA amesema amechukua uamuzi huo kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya siasa na amepania kuwaletea maendeleo ya kweli wana Kibaha akibahatika kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha amewataka wapiga kura kujiepusha na watu wanaokuja Kibaha nyakati za uchaguzi kwa lengo la kutaka kupata nafasi za kisiasa, ilihali wakiwa sio wakazi na wenyeji wa Kibaha na hivyo kushindwa kuelewa kiini cha matatizo ya Kibaha.

Wakati mgombea aliyejitokeza kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM anajinadi, Nao UKAWA hawapo nyuma katika kuhakikisha wanatoa upinzania mkali kwa CCM ambapo Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa CHADEMA,BW.FADHILI NGONYANI ameelezzea nia yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ya Machinjioni.

BW.NGONYANI amesema wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya ukweli ya kimfumo nchini ili kuwezesha kuharakisha harakati za kimaendeleo kwa jamii ya watanzania ambao kwa sasa wanaishi katika umaskini mkubwa.