Afya
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarika vizuri
baada ya kufanyiwa upasuaji wa tensi dume katika Hospitali ya John
Hopkins iliyoko Maryland Marekani tarehe 9/11/2014. Tayari Mhe. Rais
amenza kufanya mazoezi kuashiria hivi karibuni atarejea nyumbani na
kuendelea kuchapa kazi. Tuendelee kumuombea kwa Mungu. Aliyesimama ni
Mwakilishi wa Tanzania nchini Marekani Balozi Liberata Mulamula
aliyefika hospitalini kumjulia hali. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)
|