Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Ghalib Mohamed Bilal
akipata maelezo ya Historia, Muundo, Kazi na utendaji wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutoka kwa Afisa Habari wa Bunge Bw. Prosper Minja mara
kiongozi huyo alipotembelea banda la Bunge katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo
lijini Dar es Salaam ambapo kuna
maonesho ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano. Taasisi mbalimbali za serikali
na binfsi zinaonesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 50
Muungano. Dkt. Bilal aliipongeza Ofisi ya Bunge kwa kutunza kumbukumbu hasa
pale alipoambiwa kwamba Ofisi hiyo inazo
Taarifa rasmi za Baraza la Kutunga Sheria za Mwaka 1926.
|