UKAWA watoka ukumbini:Aprili 16, 2014 ni siku ambayo iliingia katika historia ya Tanzania. Hii ni kutokana na kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi linalounga mkono uwepo wa serikali tatu (UKAWA) kuamua kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma na kutoka nje ya ukumbi kwa madai ya kudhalilishwa na kundi linalounga mkono uwepo wa serikali mbili ndani ya Muungano.