Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (katikati) akipokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kiwete Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 kutoka kwa Balozi wa Nigeria nchini Marekeni Profesa Adebowele Adufye. Tuzo hiyo imetolewa tarehe 9 Aprili 2014 katika Hotel ya St. Regis jijini Washington DC. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye alikuwa nchini Marekeni kikazi na hivyo akaalikwa kwenye hafla hiyo. |