.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, March 4, 2014

Wajumbe Bunge Maalum waaswa kupunguza jazba


Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Pandu Ameir Kificho akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba alipowasili katika ukumbi wa Bunge l Mjini Dodoma kushoto kwake ni Bw. Mohamed Mbwana, katikati ni Rufai Said Rufai na Kulia kwa Mwenyekiti ni Bw. Heri Khatibu.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia na Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi Charles Tizeba wakiwasili katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.

Baadhi ya wa Bunge Maalum la Katiba waliohudhuria katika semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya wakati wa Muendelezo wa Vikao vya Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi.

Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia akitoa mapendekezo juu ya taratibu za kupiga kura katika kufanya marekesho ya kanuni zitakazotumika katika Bunge Maalum la Katiba, wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akitoa mapendekezo yake kuhusu taratibu za upigaji kura unaoangalia maridhiano ya misingi ya kidemokrasia .Kulia ni Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum Prof. Mark Mwandosya na mbele ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa.wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba   Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi(Kushoto) leo mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiongea na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na kuwataka kuzingatia maadili na lugha fasaha katika kikao hichi ili kufikia lengo linalotazamiwa kwa maslahi ya Taifa.Wakati wa semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Vuai Ally Vuai akiongea katika semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kuwataka wajumbe kufuata yale aliyoyasema Waziri Mkuu ya kuzingatia Staha ya Lugha katika Vikao vya Bunge Maalum la katiba Mjini Dodoma. (Picha kwa hisani ya Hassan Silayo)