.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, March 26, 2014

Spika Makinda aapishwa, Kamati ya Uongozi yakutana

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anne Semamba Makinda
akila kiapo cha Ujumbe wa Bunge Maalu.

Mwenyekiti Wa Bunge Maalum Mhe Samuel Sitta akimwapisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
Mhe. Sitta akimkabidhi Mhe. Makinda vitendea kazi

Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum, Wajumbe wasiozidi watano wa kuteuliwa, Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum pamoja na mambo mengine inajukumu la kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.




Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana leo.





Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.