.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, March 21, 2014

Kikwete: Kauli mbiu na Vitendo vyenu vikiwa ni TANZANIA KWANZA majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amasema Serikali ya CCM inaouwezo wa kuzirekebesha kero za Muungano na nchi kubaki ya serikali mbili badala ya tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Rais Kikwete leo amelihutubia Bunge Maalum na kusema kuwa serikali tatu ni lazima ziwe na msingi wake jambo amblo si rahisi kwani ni lazima nchi washirika ziichangie uwepo wake.


Iwapo wajumbe wataamua kuwepo kwa serikali tatu, kwa maoni yake (Rais) amesema huo ni uamuzi ambo watakuja kuujutia baada ya muda si murefu. Kuuvunja muungano na kujitenga ni kosa ambalo halitaishia hapo tu bali ni chanzo cha mifarakano ya ndani. Kuamua serkali tatu ni kuamua kuuvunja muungano rasmi, alisema Rais huku akishangiliwa na wajumbe.

Akizungumza mjini Dodoma ambapo viongozi wote wa Kitalfa walikuwepo, Mheshimiwa Kikwete amesema hoja zilizojitokeza kwenye Rasimu ya Katiba kama vile wapiga kura kumkataa mbunge wao, wabunge kutokuwa mawaziri, mbunge kuikosa nafasi kwa kuwa nje ya Bunge kwa zaidi ya miezi sita (kwa kufungwa au kwa kuugua) na ukomo wa ubunge kuwa ni mambo yanayohitaji tafakuri ya kina kabla ya kufanya maamuzi.

Ikumbukwe kuwa Katiba na hasa ikiwa nzuri ni chombo kitakachodumu kwa muda mrefu na kuwataka wajumbe kujituma katika kuiandika kwani ikiwa ya manufaa na yenye maslahi kwa taifa majina ya wajumbe hao yataandikwa kwa wino wa dhahabu. Mkifanya vibaya mtapewa lawama stahiki, aliwaonya Wajumbe. Amwewakata wajumbe wote wawe na kauli mbiu: TANZANIA KWANZA

Rais alimalizia hotuba yake kwa kumpongeza Mzee Pandu Ameir Kificho kwa kuendesha Bunge Maalum akiwa Mwenyekiti wa Muda bila kanuni za kumwongoza. Pia amewata wajumbe kuongeza kasi, kupunguza jasba na kuwa na staha ili kutowakatisha tamaa watanzania, huku akimwagia sifa Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samweli Sitta kwa umaahiri wake wa kuongoza vikao.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salama ya heshima kutoka Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride liliandaliwa na Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutuba Bunge Maalum la Katiba wakati wa sherehe za uzinduzi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali akiwasili katika ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.



Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume akiwasili katika ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.



Rais Mstaafu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia) na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu wakijadiliana jamba nje ya ukumbi wa Bunge kabla hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.