THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa
A. Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa, aliyefariki
leo tarehe 25 Machi, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Pokea rambirambi zangu za dhati na masikitiko makubwa kufuatia kifo cha
Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa kwa
Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi. Marehemu John
Gabriel Tuppa amefariki leo tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya
Tarime.
Rais pia amemwomba Mhe. Ghasia amfikishie salamu za
pole kwa Mke wa Marehemu,Watoto na
Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao. Rais amesema, anaelewa
machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu kwani wamepoteza nguzo imara
waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.
“Hakika tumempoteza kiongozi mchapakazi ambaye amekuwa
akijituma na kuwatumikia Wananchi wake
hadi dakika za mwisho za uhai wake.
Pengo aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi kuzibika kamwe lakini hatuna
budi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho ya Marehemu mahali pema peponi” Amina.
Taratibu na maandalizi ya mazishi zinafanywa kwa
ushirikiano wa Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI.
Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na
katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma
kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto
watano.
Mwisho!
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25
Machi,2014