Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samwel Sitta akimkaribisha Bungeni Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ili awasilishe rasmi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum kwa mujibu wa kanuni ya 7(1)h ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014.
Rasimu
yaainisha vipaumbele vya uongozi
Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Sinde
Warioba, ameliambia Bunge Maalum linaloendelea mjini Dodoma kuwa Rasimu ya
Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na Wabunge.
Jaji Warioba amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye Bunge
kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya Bunge hilo kunalifanya Bunge kushindwa
kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya Bunge.
Amesema Mawaziri watateuliwa na na Rais na watakuthibitishwa na
Bunge . Aidha, rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata
kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .
Rais, mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi
anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa
kiti hicho aliyeshindwa na shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja, ilisema
sehemu ya taarifa ya Jaji Warioba.
Mwenyekiti Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo
na ukomo wa wabunge kwa vipindi vitatu mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki
wa majimbo na hii itasaidia kuimarisha uwajibikaji.
Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala
yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa na
vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.
Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu
Waziri au wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.
Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, akiwasilisha rasmi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum
Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, akiwasilisha rasmi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum
Wajumbe wa Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.
Wajumbe wa Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.
Jaji Warioba akiendelea kuiwasilisha Rasimu
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Augustino Ramadhani akitoa neon la shukrani kwa Wajumbe wa Bunge Maalum.