Hawa ni Bwana Joseph Lyimo mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Mzumbe (kulia) na Bi. Zuwena Ibrahim mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Tumaini ambao wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la vijana
litakalofanyika Lilongwe, Malawi kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2013 ambapo
pamoja na mambo mengine watazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha vijana mapema
katika vyombo vya maamuzi.
Rais wa CPA Kanda ya Afrika na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb), akiwakabidhi Waheshimiwa Wabunge hao wateule bendera ya Tanzania akiwataka waiwakilishe na kuipeperusha vema bendera hiyo ya Tanaznia katika Bunge la Vijana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Mhe. Mussa Zungu Azzan, (Mb) na Kamishna wa Bunge Mhe. Beatrice Shilukindo (Mb).
Wahadhiri waandamizi kutoka katika Vyuo Vikuu vya Mzumbe na Tumaini walioambatana na wanafunzi wao katika hafla ya kuwaaga. Hapa wapo kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Makinda.
Spika Makinda akimpa mkono wa heri na baraka Mhe. Zuwena kama ishara ya kuwaaga vijana hao
Mhe. Joseph Lyimo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya hafla hiyo ambapo ameahidi kuiwakilisha Tanzania vema.
Wateule hao wakiwa na ndugu, jamaa na marafiki zao
Zawadi kutoka chuo Kikuu cha Mzumbe