.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, August 20, 2013

Mzumbe na Tumaini kupeperurusha bendera ya Tanzania Bunge la Vijana CPA Malawi


Hawa ni Bwana Joseph Lyimo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (kulia) na Bi. Zuwena Ibrahim mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini ambao wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la vijana litakalofanyika Lilongwe, Malawi kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2013 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha vijana mapema katika vyombo vya maamuzi.Rais wa CPA Kanda ya Afrika na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb), akiwakabidhi Waheshimiwa Wabunge hao wateule bendera ya Tanzania akiwataka waiwakilishe na kuipeperusha vema bendera hiyo ya Tanaznia katika Bunge la Vijana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb),  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Mhe. Mussa Zungu Azzan, (Mb) na Kamishna wa Bunge Mhe. Beatrice Shilukindo (Mb).
Wahadhiri waandamizi kutoka katika Vyuo Vikuu vya Mzumbe na Tumaini walioambatana na wanafunzi wao katika hafla ya kuwaaga. Hapa wapo kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Makinda.
 Spika Makinda akimpa mkono wa heri na baraka Mhe. Zuwena kama ishara ya kuwaaga vijana hao
Mhe. Joseph Lyimo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya hafla hiyo ambapo ameahidi kuiwakilisha Tanzania vema.
 Wateule hao wakiwa na ndugu, jamaa na marafiki zao

 Zawadi kutoka chuo Kikuu cha Mzumbe