.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, May 31, 2013

MPIGANAJI ERNEST ZULU AZIKWA KIJIJINI KWAO SONGEA LEO

 
     Mwakilishi wa Spika wa Bunge ambaye pia ni Kamishna na Mbunge wa Mafia Mhe. Abdul Karim Shah akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya Afisa Habari Mkuu wa Bunge marehemu Ernest Zulu yaliyofanyika katika kijiji cha Ndilima, Peramiho mkoani Songea leo.


Mwakilishi wa Katibu wa Bunge ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Jossey Mwakasyuka akisoma wasifu wa marehemu Ernest Zulu.


Katibu wa Bunge Mstaafu Mzee George Mlawa  akitoa salamu za rambirambiBaada ya salamu hizo, ndipo Padre Fidelis Mligo wa Abisiya ya Peramiho akaongoza ibada ya Misa Takatifu na mazishi ya mtumishi huyo wa Bunge


Mkuu wa Wilaya ya Songea Ndugu Joseph Mkirikiti  (wa pili kushoto waliokaa) aliiwakilisha serikali katika mazishi hayo.


Waombolezaji kutoka Ofisi ya Bunge


Dada yake marehemu akiwa amepoteza fahamu wakati wa mazishi ya kaka yake.Mwakilishi wa Spika wa Bunge Mhe. Abdul Karim Shah akiweka udongo kaburini kushiria safari ya mwisho ya Afisa Habari Mkuu wa Bunge marehemu Ernest Zulu leo