Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya
Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa
mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika. Pongeli
hizi zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo
kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete
pamoa na watanzania kama wapenda amani barania Afrika. Hii ni kutokana na
viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la M23,
migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa
Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini
nay imepongezwa. Bunge la Tanzania limewkilishwa na Spika wa Bunge ambaye
ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe.
Pauline Gekul, na Mhe Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe.
Prudenciana Kikwembe.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo. |
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa |
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo
|
Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja
washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR
|
Wadau
Light moments