Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth
Natongo Zziwa akifungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa
wabunge wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya
ambayo hafanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda,
Bunrundi, Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi
haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini
Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote ambao
wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.
|