Tanzania
Tanzania Bunge Sport Club Netball
imefanikiwa kuwa kileleni baada ya kuitandika timu ya muungano ya Jumuiya na
Bunge la Afrika Mashariki kwa mabao 49-9. Katika mchezo mkali wa mashindao ya
michezo ya mabunge yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya, timu ya Tanzania
imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachakaza bila huruma wenyeji wao Kenya
kwa mabao 51-25. Mashindano haya ambayo huandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki
kwa kushirikiana na Bunge la Afrika Mashariki kwa lengo la kudumisha
mshikamano, yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 14 Disemba 2012. Tayari Tanzania
imeweka kibindoni mabao 100, mtaji ambo si rahisi kfikiwa na timu nyingine
zilizosalia.
Tayari Tanzania Bunge Sports Club
Football wameshajihakikishia kuingia nusu fainali baada ya kutoa adhabu kali kwa timu za Kenya
na Rwanda. Kwenye mechi yake na Kenya,
Tanzania ilijipatia mambo 5-0. Aidha kwenye mchezo wake na Rwanda Tanzania
iliifunga Rwanda mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa City.
Awali Kenya Bunge Sports Club
Football ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Mashariki katika mchezo uliopigwa kwenye
Uwanya wa Nyayo mbele ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth
Natongo Zziwa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo. Aidha
kwenye mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki Uganda ilijipatia mabao 2 -1,
huku Rwanda ikijipatia magoli 2-0 dhidi ya Kenya.
|