Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Napoli, Italia na kulakiwa na mwenyeji wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dkt James Nsekela leo. Mhe. Makinda yuko nchini Italia kuhudhuria mkutao wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa unaohusu jinsi ya kukabiliana na ukuaji wa miji ulimwenguni. Hivyo zinahitajika juhudi za makusudi ili kuweka mipangilio stahihiki katika miji ya Tanzania hususan majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji. Ni hivi majuzi ilitangazwa kuwa Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika. Ujumbe wa Tanzania katika mkjutano huu unaongozwa na naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Goodluck Ole Medeye.Mkutano huo utaanza kesho tarehe 2 na kuhitimishwa tarehe 6 septemba 2012.