.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Saturday, March 24, 2012

MESSAGE ON THE INTERNATIONAL DAY FOR THE RIGHT TO THE TRUTH CONCERNING GROSS HUMAN RIGHTS VIOLATIONS AND FOR THE DIGNITY OF VICTIMS 24 March 2012

Today we pay tribute to the memory of Monsignor Oscar Arnulfo Romero, who was murdered in El Salvador on this day in 1980 for refusing to be silent in the face of violence, abuse and injustice.
The International Day for the Right to the Truth Concerning Gross Human Rights Violations and for the Dignity of Victims is also a time to laud the brave individuals across the world who have devoted their lives to the protection and realization of human rights despite the many grave risks that their work all too often entails.
The dramatic and transformational events of the past year, marked by widespread popular uprisings against long-entrenched dictators, showed yet again the acute need to preserve and reveal the truth about human rights violations committed during periods of repression and conflict. To deny victims this vital knowledge is to deny them justice, dignity and recognition of – as well as reparations for – their suffering and loss.
The implications reverberate well beyond individuals who have been directly affected by attempts to cover up human rights abuses. The rights to truth and justice are central to ending impunity for gross violations of human rights. In cases of enforced disappearance, families have the right to know the fate and whereabouts of their loved ones. In all instances, honouring this right puts others on notice that violations cannot stay hidden for long.
I am proud that the United Nations supports a range of truth-seeking mechanisms that can play a powerful role in documenting gross human rights violations, including truth and reconciliation commissions, international commissions of inquiry and fact-finding missions. These are central to our quest for justice and stability.
I also welcome the recent decision by the United Nations Human Rights Council to appoint a new Special Rapporteur on the promotion of truth, justice, reparation and guarantees of non-recurrence.
On this International Day, let us work to help all victims realize their right to truth and to protect all those who fight to see the truth prevail.
By the courtesy of Fullshangwe blog

Wednesday, March 21, 2012

Elimu kwa vitendo shuleni iko wapi?

Na Prosper Minja

KATIKA moja ya hotuba za hayati  Baba wa Taifa Mwlimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuna baadhi ya mambo hapa nchini ukitaka kuyahoji lazima uwe na moyo mgumu kama wa mwendawazimu hivi.   Kwa sasa moja ya mambo hayo ni elimu: elimu ya awali; elimu ya msingi; elimu ya sekondari; elimu ya vyuo. Zamani ili shule ihesabike  na hata kusajiliwa kama shule kuna mambo mengi yalihitajika likiwemo la uwanja wa michezo na shamba la shule. Siku hizi ni dhambi ya mauti kuzungumzia shamba la shule tena mzazi akikuskia achilia mbali mwalimu! Mwanafunzi ndiyo kabisa atatamani umwagiwe tindikali!
Siku hizi mtoto anafanyiwa kila kitu awapo shuleni. Kuna watu wa kufanya usafi ndani na nje ya vyumba vya madarasa, , kupika, basi la kumbeba na kurudisha nyumbani, akifika nyumbani kuna msaidizi/mfanyakazi wa nyumbani wa kumfulia hadi nguo za ndani, kumpikia, kumtandikia kitanda na kunyooshea nguo. Shuleni shamba darasa tena hakuna. Zamani katika orodha ya vifaa vya kwenda navyo shuleni jembe kilikuwa kifaa kimojawapo. Siku hizi dhubutu! Kiwanja cha michezo si sharti muhimu tena. Hali hii iko tangu shule ya awali hadi chuo kikuu! Ni dhahiri maandiko haya hayatabadilisha chochote kwa wakati huu lakini yataonekana ya maana Wachina watakapoanza kuchangamkia hata kazi za majumbani hapa Tanzania kwani wao wamefundishwa maana ya kazi kwa vitendo.
Serikali, wazazi, wadau wako wapi kudai na kuhimiza kazi za mikono katika shule zetu? Shule yoyote kabla ya kusajiliwa ioneshe japo shamba darasa mahali wanafunzi watajifunza kwa vitendo kupanda na kuvuna mchicha. Wanafunzi wafundishwe kufanya usafi kwa vitendo kwa mfano kufagia darasa, kuokota takataka, kukata kucha, kuosha sahani yake anapomaliza kula,  kutoa buibui na nyinginezo. Wakiwa majumbani wajifulie ngou zao wenyewe, wafanye usafi, wajifunze kupika, wanyooshe nguo zao wenyewe, watengeneze bustani na kuzimwagilia inapobidi, wahimizwe maswala ya kiroho, kwa kifupi wafundishwe kuwajibika.
Jeshi la Kujenga Taifa ndilo lilikuwa limesalia ili kuziba ombwe hili. JKT halipo tena. Na hata ikitokea likawepo halitokuwa tena kama la opereshini miaka 30 (waliopita jeshini wanaelewa operesheni).   Ole wetu! Ole wa Taifa hili!. Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dkt. Ndalichako alinukuliwa akilalamika kwamba wanafunzi waliandika mashairi ya Bongo flavor kwenye mitihani! Kumbe waandike nini? Nyimbo za makuzi shuleni siku hizi hakuna tena. Nyimbo za kizalendo na ukakamavu ni historia mashuleni! Kibaya zaidi hata Wimbo wa Taifa  umebaki kuchezwa mkanda tu uliorekodiwa halafu  wanafunzi kusikiliza! Mustakabali wa Taifa uko wapi! Tusipojenga msingi imara tusishangae nyumba kuporomoka kwani Walatini wanasema volenti non fit injuria! (lakijitakia halina madhara). Tumeyata wenyewe!
Tuna wakaguzi waliosoma. Hivi hawa wanakagua nini? Mwandiko mzuri? Mwalimu kumaliza silabasi? Wadau nisaidieni. Mada ni pana. Mtoto huyu akimaliza shule (darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, shahada ya kwanza) anakuwa ni mzigo usiobebeka pande zote. Si kwa wazazi, si kwa serikali! Hawezi kufanya kitu chochote! Hajafundishwa kufanya hivyo! Hajalelelwa katika mazingira hayo! Hana pa kuanzia. Dhana ya kilimo kwanza kwake ni msamiati usio na mashiko. Likitokea la kutokea kwamba mzazi amefariki dunia huu unakuwa ni mwanzo wa mwisho wa mtoto huyu! Ataanza kujioanisha na mazingira  yatakayomfaa (to search for identity). Atayapata mazingira hayo  au kwa watumia dawa za kulevya kwa wavulana au kwa kupiga umalaya kwa wasichana. Hapa tusiulizane madhara yake nini.
Laiti mtoto huyu angelikuwa anajua kujitegemea japo kidogo tu angeyamudu maisha. Angekuwa mnyenyekevu. Kwa bahati mbaya kila mtoto anaota kwenda Ulaya tena kwa gharama yoyote ile. Mzazi atafanya kila linalowezekana na lisilowezekana, mtoto atahonga hata visivyohongeka ili mradi aende Ulaya! Kufanya nini? Sina jibu.
Sera ya elimu iangaliwe upya. Shule zote (binafsi na serikali) ziwekewe vigezo. Tusiogope kujifunza kutoka mahali pengine. Kwa mfano shule za seminari zinaongoza kwa kufanya vizuri. Lakini hapa ni mahali wanafunzi wanafanya kazi zote peke yao. Wana mashamba yao wanayolima na kuvuna wenyewe, wanafanya usafi wa mazingira na vyumba vya madarasa yao, kwa kifupi wanajitegemea wakiongozwa na nidhamu ya hali ya juu. Haijawahi kutokea mtoto aliyemaliza masomo katika shule hizi akawa tegemezi kiasi cha kutobebeka. (kwa ujasiri naruhusu changamoto/challenge kwa hili kutoka wa mtu yeyote). Huu ni ushahidi kwamba inawezekana.
Tujenge msingi imara ili kuwa na taifa imara.
0713 123 254
www.prince-minja.blogspot.com
 (Tanzania Daima, Na. 2665, Machi 21, 2012, uk 20)

Wednesday, March 14, 2012

Press Release
Tanzania Commission for Universities regrets to inform the Public that it has received news that it does recognize Japan Bible Institute and so the Institute is legally operating in Tanzania. The information about Japan Bible Institute’s  graduation has been reported on the Guardian ISSN 0856- 5422 ISSU No 5384 of Monday March 12th 2012 front page with the heading “Japan Institute Honours Mengi, others for serving humanity” and on ITV News Bulletin of the same day.

The two sources quote the Director of Japan Bible Institute for Africa Dr. Paul Zemu Shemsanga making a remark on Saturday at the Institutions second Graduation ceremony to honour the people who have worked to serve humanity. Dr. Shemsanga said his Institute is recognized by the Tanzania Commission for Universities (TCU) which is not true.

Tanzania Commission for Universities’ position is that Japan Bible Institute is not recognized as a Higher Education Institution and thus any awards conferred by Japan Bible Institute whether honorary or academic will not be valid or recognized in Tanzania.

Thus any person who volunteers to receive such awards does so on his/her own will and risks as to the status of the award in Tanzania.
Released by:
Executive Secretary
Tanzania Commission for Universities
P.O.Box 6562
Dar es Salaam

Saturday, March 10, 2012

Ofisi ya Bunge yapokea rasmi nyumba mpya ya Spika kutoka Pacha Building Construction Compamny

   Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto)
akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na
Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas Wambura mara tu kabla
 ya makabidhiano rasmi ya nymba atakayokuwa anatumia
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoko
 eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.


Muonekano wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo
litakuwa makazi ya Spika yeyote atakayeliongoza Bunge
la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 na limegharimu
 takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya
Spika wa Bunge Dodoma



Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction
Company ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban
Mwatawala (kulia) akitoa maelezo ya ujumla kabla ya
kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya Bunge katika jengo hili.
Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha
Bw. Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na
Teknolojia ya Mawasiliano wa Bunge Bw. Siegfied Kuwite,
 na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John Joel.

 

Bw. Siegfried Kuwite akitia saini makabidhiano hayo kwa
niaba ya Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mshitiri (client)
wa jengo.


Bw.Shaban  Mwatawala akitia saini makabidhiano hayo
kwa niaba ya Pacha Building Construction Company.


Bwana Mwatawala akimkabidhi  Msanifu Majengo
M. F. M Msangi (kulia) anyewakilisha Wakala wa Majengo ya
 Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa
Mradi huu.



Mlango wa mbele wa jengo.


Ngazi ndani ya jengo ambalo lina vyumba vinne
vya kulala, sehemu ya mapumziko, sehemu ya chakula,
maktaba na jiko.





Mazingira yanayolizunguka jengo.
 

Wadau katika zoezi zima la makabidhiano



















End


Tuesday, March 6, 2012

Maandalizi kabambe mkoa mpya wa Njombe


 Mbunge wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge
la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisaini
kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Idundilanga.

Maandalizi kabambe mkoa mpya wa Njombe
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kutangaza nia ya kuugawa mkoa wa Iringa ili kuwa na mikoa miwili yaani mkoa wa Iringa na Mkoa wa Njombe, wananchi wa mkoa mpya wa Njombe hawalali hadi kieleweke. Kwa kujituma kunakostahili kuwa mfano wa kuigwa na kwa ushirikiano usiojali imani, kabila au itikadi za kisiasa wamedhamiria kuujenga mkoa wao huo kwa kiwango cha hali ya juu. Mbinu wanazotumia ni kupiga vita umaskini kwa kuchapa kazi hususan za kilimo cha mazao ya chakula (mahindi, matunda, viazi,) na biashara (miti ya mbao), kupiga vita ujinga kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya awali na msingi pamoja na kila kata kuwa na shule ya upili, na kupiga vita maradhi kwa kujenga zahanati na vituo vya afya.  Wakionesha ari na msukumo mkubwa kwa Mbunge wao Mhe. Anne Semamba Makinda aliyewatembelea wananchi hao hivi karibuni, wananchi hao wanajivunia tabia yao ya kupenda kufanya kazi kwa bidii na kujituma, ardhi yenye rutuba walio nayo pamoja na ukanda wanamoishi wa nyanda za juu kusini wenye mvua za kutosha nyakati zote.
Akizungumza nao mbunge huyo aliwasisitizia kujipanga vizuri ili kuzifaidi fursa zitakazotokana na uchimbaji wa mkaa wa mawe pamoja na chuma katika migodi ya Ludewa na Liganga ambayo utekelezaji wake tayari uko katika hatua za kuanza uchimbaji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli ambazo wananchi wa Njombe wanashiriki.
Mbunge akikagua daraja la Luponde-Kisilo la mto Hagafilo linalojengwa kwa nguvu za wananchi.

Daraja la Luponde- Kisilo


Ujenzi zahanati ya Kisilo


Pamoja na mvua kubwa wananchi wanataka kusikia Mbunge wao anawaambia nini kuhusu maendeleo yao

Maandalizi ya kiwanja cha ujenzi wa zahanati ya Matalawe (SIDO)

Baada ya kumalizika ujenzi wa shule juhudi sasa zinaelekezwa kwenye ujenzi wa nyumba za waalimu.

Baadhi ya nyumba za waalimu katika kijiji cha Ikisa.

Wananchi kwenye mkutano.

Tatizo linalowakumba wakulima ni kutozingatiwa kwa vipimo katika mazao yao. Hii ni rumbesa ya viazi ambayo inawaumiza sana wakulima na hivyo kuiomba serikali iingilie kati.

Kilimo cha mahindi



 Mwananchi akitoa maoni yake katika kitongoji cha NHC




 Kituo cha Afya Idundilanga


     Siasa si ugomvi: Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Wilaya ya Njombe Bw. Alatawa Nyagawa akisalimia na Mbunge wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge mjini Njombe wakati wa ziara ya Mbunge huyo.

Katibu wa CHADEMA (W) Njombe Bw. Nyagawa akisalimiana na wananchi wakati wa ziara ya Mbunge

Baadhi ya madiwani na viongozi walioambatana na Mbunge




 Mwananchi akiomba ufafanuzi wa vifungu vya Katiba ya nchi: Mwamko mkubwa ulioko vijijini.