Mbunge wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Idundilanga. |
Maandalizi kabambe mkoa mpya wa Njombe
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kutangaza nia ya kuugawa mkoa wa Iringa ili kuwa na mikoa miwili yaani mkoa wa Iringa na Mkoa wa Njombe, wananchi wa mkoa mpya wa Njombe hawalali hadi kieleweke. Kwa kujituma kunakostahili kuwa mfano wa kuigwa na kwa ushirikiano usiojali imani, kabila au itikadi za kisiasa wamedhamiria kuujenga mkoa wao huo kwa kiwango cha hali ya juu. Mbinu wanazotumia ni kupiga vita umaskini kwa kuchapa kazi hususan za kilimo cha mazao ya chakula (mahindi, matunda, viazi,) na biashara (miti ya mbao), kupiga vita ujinga kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya awali na msingi pamoja na kila kata kuwa na shule ya upili, na kupiga vita maradhi kwa kujenga zahanati na vituo vya afya. Wakionesha ari na msukumo mkubwa kwa Mbunge wao Mhe. Anne Semamba Makinda aliyewatembelea wananchi hao hivi karibuni, wananchi hao wanajivunia tabia yao ya kupenda kufanya kazi kwa bidii na kujituma, ardhi yenye rutuba walio nayo pamoja na ukanda wanamoishi wa nyanda za juu kusini wenye mvua za kutosha nyakati zote.
Akizungumza nao mbunge huyo aliwasisitizia kujipanga vizuri ili kuzifaidi fursa zitakazotokana na uchimbaji wa mkaa wa mawe pamoja na chuma katika migodi ya Ludewa na Liganga ambayo utekelezaji wake tayari uko katika hatua za kuanza uchimbaji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli ambazo wananchi wa Njombe wanashiriki.Mbunge akikagua daraja la Luponde-Kisilo la mto Hagafilo linalojengwa kwa nguvu za wananchi. |
Daraja la Luponde- Kisilo |
Pamoja na mvua kubwa wananchi wanataka kusikia Mbunge wao anawaambia nini kuhusu maendeleo yao |
Maandalizi ya kiwanja cha ujenzi wa zahanati ya Matalawe (SIDO) |
Baada ya kumalizika ujenzi wa shule juhudi sasa zinaelekezwa kwenye ujenzi wa nyumba za waalimu. |
Baadhi ya nyumba za waalimu katika kijiji cha Ikisa. |
Wananchi kwenye mkutano. |
Tatizo linalowakumba wakulima ni kutozingatiwa kwa vipimo katika mazao yao. Hii ni rumbesa ya viazi ambayo inawaumiza sana wakulima na hivyo kuiomba serikali iingilie kati. |
Kilimo cha mahindi |
Mwananchi akitoa maoni yake katika kitongoji cha NHC |
Kituo cha Afya Idundilanga |
Katibu wa CHADEMA (W) Njombe Bw. Nyagawa akisalimiana na wananchi wakati wa ziara ya Mbunge |
Baadhi ya madiwani na viongozi walioambatana na Mbunge |
Mwananchi akiomba ufafanuzi wa vifungu vya Katiba ya nchi: Mwamko mkubwa ulioko vijijini. |