Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza, wakifuatilia kwa makini hoja kutoka kwa wajumbe wanaowania uwenyekiti wa Dunia wa chama hicho. Kutoka Kushoto Ni Ndg. Emmanuel Mpanda, anayemwakilisha katibu wa Bunge, Naibu Spika Mhe. Job Ndugai, Mhe. Zungu, Mhe. Beatrice Shelukindo, Mhe. Zitto Kabwe na Mhe. Maua Daftari. Jumla ya wagombea watatu kutoka, Uingereza, Pakistani, na visiwa vya Samoa, wanawania kiti hicho. |