Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Dianne Corner ofisini kwake Dodoma leo. Balozi Corner pamoja na mambo mengine alizungumzia Mkutano wa Chama cha Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CPA) utakaofanyika Uingereza mapema mwezi ujao. Chama hicho kinatimiza miaka mia moja tangu kianzishwe mwaka 1911.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mhe John Momose Cheyo, Balozi Dianne Corner, Mhe, Naibu Spika na Mwenyekiti wa kikao, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa A. Zungu.
Balozi Corner akiagana na Mhe. Kairuki
Prosper Minja-Bunge