.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, June 10, 2011

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Naibu Waziri Mkuu wa Ireland wamtembelea Spika Makinda





 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge la Afrika Mashariki walipomtembelea Ofisini kwake Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha ripoti ya mwaka. Kutoka kushoto ni Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Janeth Mmary na Mhe. Amani W. Kabouru.
Spika Makinda akiwa kwenye mazungumzo ofisini kwake Dodoma leo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Mhe. Eamon Gilmore. Mhe. Gilmore ameipongeza Tanzania kwa kuchukua hatua za kuandika Katiba Mpya.
 Ujumbe wa Msafara wa Mhe. Gilmore ukifuatilia kikao hicho kwa umakini. Kutoka kushoto ni Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan, Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid) Bwana Brendan Rogers na Mshauri wa Mhe. Gilmore Bi. Jean O’Mahony.

 Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi yachupa mbili za  Mvinyo (Presidential na Ambassador)  unaotengezwa Tanzania kwa zabibu zinazozalishwa Tanzania  katika Mkoa wa Dodoma.
 Mhe. Gilmore akiitazama zawadi ya saa ya ukutani yenye picha ya jingo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 Mhe. Gilmore akimkabidhi Mhe. Spika zawadi

Spika akiagana na mgeni wake