.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, May 31, 2011

Kuelekea Katiba Mpya: Spika Makinda akutana na BAKWATA, Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania

     Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba akimkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Ofisini kwakeDar es Salaam leo. Spika Makinda alifanya ziara hiyo kwa lengo la kupanua mjadala wa maudhui ya kuundwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya. Kulia kwa Mufti ni Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaji Suleima Lolilya na kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki. Aidha Spika Makinda pia alikutana na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania kwa mwaliko wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kupokea maoni na ushauri kuhusu uundwaji wa chombo hicho cha kukusanya maoni.

     Mufti Mkuu akiendesha Dua maalum kabla ya mjadala kuanza.


      Viongozi wa BAKWATA wkifuatilia mjadala.

      Mufti akitoa maoni yake.

  Spika Makinda akiushikuru uongozi mzima wa BAKWATA na kuwaahidi kuwa maoni na ushauri wao vitazingatiwa

     Spika Makinda (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania katika Hotel ya Courtyard, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekit wa Baraza na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza.

     Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji akimshukuru Mhe. Spika kwa uamuzi wake wa busara wa kukutana na wadau mbalimbali ili kupata muafaka wa kitaifa wa upatikanaji wa katiba mpya


   Wajumbe wa Baraza wakifuatilia mjadala


   Baraza la vyama vya Siasa Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Anne Makinda (katikati)
Picha na Prosper Minja-Bunge