.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, May 23, 2011

Matukio Bungeni


 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Anne Makinda akifafanua kwa wanahabari mwenendo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12 mara baada ya kufunga mkutano wa vyombo vya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali barani Afrika Ubungo Plaza Dar es Salaam, jana.


Mwenyekiti wa Kamati yaBunge ya Hesabu za Serikali Mhe. John Momose Cheyo Mb, akimkabidhi Mhe Spika zawadi iliyotolewa na wajumbe wa mkutano huo.



 Spika Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation, TPSF) Bi Esther Mkwizu akitoa maoni ya makundi mbali mbali ya wadau wa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya leo katika ofisi ya Spika wa Bunge. Kushoto kwake ni Spika Makinda akimsikiliza kwa makini.
Wajumbe kutoka TCCIA na TPSF wakifuatilia mjadala
Katibu Mkuu wa Baraza la wafanyakazi Tanzania Bw, Mgaya amabaye ameongozana na viongozi waandamizi wa vyama vya wafanyakazi vya CWT, TUGHE, RAAWU, TALGWU, TUICO, TUCTA na ATE akitoa maoni kuhusu kuundwa kwa tume ya Katiba mpya leo.

 Ujumbe kutoka Muungano wa Ulaya ukiongozwa na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Bw. Nick Westcott (kati) na Mwakilishi wa Muungano huo hapa Tanzania Balozi Tim Clake (kulia) ulipomtembelea Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda (kushoto) ofisini kwake leo. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamezungumzia uboreshwaji wa bajeti na mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Na Prosper Minja-Bunge