Spika wa Bunge ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda
akifafanua baadhi ya masuali kutoka kwa wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka
Bunge la Nigeria (hawapo pichani) waliotembelea Bunge letu kwa lengo la
kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda
akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la
Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini
kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda
akiongea na Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria
walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini
kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge
ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia
kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la
Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
Juu: Kiongozi
wa Msafara wa Ujumbe kutoka Tume ya Utumishi ya Bunge la Nigeria Mhe. Yepwi
Stephen Dako akiuliza namna ambavyo Tume ya Bunge la Tanzania husimamia
Watumishi wa Bunge la Tanzania katika kuleta ufanisi kazini wakati walipokutana
na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo wa tume ya Nigeria upo nchini
kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge.