.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, September 8, 2015

Spika Makinda akutana na Tume ya Utumishi wa Bunge ya Nigeria


Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akifafanua baadhi ya masuali kutoka kwa wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria (hawapo pichani) waliotembelea Bunge letu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.

 
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.

Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
 Juu: Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Tume ya Utumishi ya Bunge la Nigeria Mhe. Yepwi Stephen Dako akiuliza namna ambavyo Tume ya Bunge la Tanzania husimamia Watumishi wa Bunge la Tanzania katika kuleta ufanisi kazini wakati walipokutana na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo wa tume ya Nigeria upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge.