.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Sunday, June 28, 2015

Taifa lamuaga Max

Taifa lamuga Donald Max

Mheshimiwa Marehemu Donald Kevin Max (58) aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geta kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Baada ya kuugua kwa muda mrefu, na kutibiwa ndani na nje ya nchi, alifariki dunia tarehe  23 Juni 2015 katika Hospitali ya Taifa Mhumbili na kuzikwa tarehe 27 Juni 2015 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza mamia ya waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa aliyukuwa Mbunge wa Jimbo la Geita Marehemu Donald Kevin Max kwenye viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo.

“Mwanadamu umetokana na  mawumbi na mavumbini utarudi” Ndivyo anavyoonekana kutamka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) wakati akiweka udongo kwenye kaburi alimopumzishwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Geita.Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Thomas Kashililah, kwa unyenyekevu mkubwa akilipamba kwa maua kaburi alimolazwa aliyekuwa Mbunge wa Geita marehemu Donald Kevin Max kwa niaba ya Muhimili wa Bunge.