THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Taifa, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Bwana Sixtus Mapunda kuomboleza
kifo cha Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, Lucy Bongele kilichotokea tarehe 2
Novemba, 2014 kwa ajali ya gari.
Ajali hiyo
ilitokea katika Wilaya ya Ngorongoro baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina
ya Land Cruiser Prado Namba T380 ADP kuacha njia na kupinduka wakati Katibu
huyo na Viongozi wenzake wa UVCCM walipokuwa wakienda kumsimika Bruno Kawasange
kuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.
Ajali hiyo iliwajeruhi viongozi wengine watano wa UVCCM pamoja na
Dereva.
“Nimepokea kwa
mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha Katibu wa UVCCM Wilaya
ya Arumeru, Lucy Bongele kilichosababishwa na ajali ya gari, wakati Katibu huyo
alipokuwa akienda kumsimika Bruno Kawasange kuwa Kamanda wa UVCCM wa Wilaya ya
Ngorongoro”, amesema Rais
Kikwete katika Salamu zake.
“Kutokana na
kifo cha hicho, ninakutumia Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa
kumpoteza mmoja wa vijana hodari na wachapakazi katika safu ya uongozi ya
UVCCM. Kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa katika safu ya uongozi wa UVCCM katika Wilaya ya Arumeru”, amesema Rais Kikwete.
“Naomba Mwenyezi
Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu
Lucy Bongele. Namwomba Mola awawezesha kupona haraka majeruhi wote wa ajali
hiyo wapone haraka ili waendelee kusaidia
UVCCM katika uongozi wake”, ameongeza
kusema Rais Kikwete katika salamu zake.
Rais Kikwete
amewaomba ndugu na jamaa wa Marehemu Lucy Bongele wawe wavumilivu na wenye
subira wakati huu wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao, na amewahakikishia kuwa
yuko pamoja nao katika kipindi chote cha maombolezo.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
4 Novemba,2014